Sura ya Pili : Tuipende shule yetu
Shule ni sehemu yajamü ambayo huwapatia watoto malezi bora. Ili Shule [we bora inapaswa kuwa na walimu na wanafunzi bora. Shule inapaswa kuwa na madarasa, vyoo, samani, mazingira safi na vifaa vya kujifunzia. Shule yenye vitu vilivyotajwa hapo juu inavutia. Katika sura hit utajifunza matendo ya kuipenda na kujivunia Shule yako. Matendo hayo hujumuisha kutunza mazingira ya shule. Vilevile, kusoma kwa bidii na kuonesha tabla njema shuleni.
Kuifahamu shule
Miongoni mwa mambo ambayo unapaswa kuyafahamu ni vitu vinavyoitambulisha Shule yako. Vitu hivyo ni mipaka ya shule, nembo ya Shule na kaulimbiu. Vitu vingine vinavyotambulisha Shule ni sare na wimbo wa shule.
Tazama picha hii, kisha jibu maswali.
Kielelezo namba 1 Mazingira ya Shule |
Maswali
1. Picha hii inaonesha nini?
2. Je, ni vitu gani unavyoviona katika picha hii?
3. Eneo hilt lina umuhimu gani katika jamii?
14. Je, ni mambo gani hufanyika katika eneo hili?
Wimbo
lmba wimbo huu, kisha jibu maswali.
Shule twaipenda, shule twaipenda
Shule twaipenda, shule twaipenda
Twawapenda walimu wetu, wanatufundisha vyema
Twawapenda viongozi wetu, wanatuongoza vgema
Twaipenda nembo ya shule yetu, inatutambulisha vyema
Tunazipenda sare zetu, zinatupa mwonekano bora
Taaluma, nidharnu na mazingira, hii ndio kauli mbiu yetu
Shule twaipenda, shule twaipenda Shule twaipenda, shule twaipenda
Μaswali
Ι. Je, ni mambo gani yanagoitambulisha shule katika wimbo huu?
2. Je, ni mambo gani mengine yanayoitambulisha shule yako?
3. Andika wimbo wa shule gako.
Κazi ya kufanya
Andika vitu vinavgobainisha mipaka ya shule gako.
Kutunza mazingira ya shule
Mazingira ya shule yanajumuisha Vitu vyote vilivyomo katika eneo la shule. Vitu hivyo ni majengo, viwanja vya michezo, bustani, miti na samani. Vitu vingine ni njia za shule, vyoo na vingine vingi. Ili mazingira ya shule yako yapendeze na kuvutia inakupasa kuyatunza vizuri. Kila mwanafunzi anapaswa kutunza mazingira ya shule yake. Unatakiwa kupanda miti na maua, kufanya usafi na kutupa takataka mahali panapostahili. Ni jukumu la kila mmoja kuchukua hatua ya kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Tazama picha hü, kisha jibu maswali.
|
Kielelezo namba 2 Usafi wa mazingira ya shule |
Maswali
l . Te, ni matendo gani unayoyaona kwenye picha?
2. Te, ni vitendo gani vya kutunza mazingira unavyovifanya shuleni kwako?
3. Taja falda za kusoma na kucheza kwenye mazingira safi na salama.
Kazi ya kufanya
Shirikiana na wenzako kufanya usafi wa darasa baada ya muda wa masomo.
Kuiletea sifa nzuri shule
Sifa nzuri ya shule inajengwa na mambo mazuri yanayofanywa na wanafunzi shuleni. Mambo kama maendeleo mazuri darasani, mazingira safi na tabla zinazofaa za wanafunzi. Juhudi za walimu huiletea sifa nzuri shule.
Soma majigambo baina ya Amani, Nuru, Upendo na Turnaini. Jibu maswali yanayofuata.
Upendo | Mmeiona, zawadi tuliyoipata? Bila mimi kucheza mpira tusingeshinda! |
Amani | Mimi ni zaidi yako. Nimeshinda kwa kuwa na tabia njema. Jina Ia shule getu litavuma zaidi nje ya shule. |
Nuru | Mimi ni zaidi yenu. Nimeshika nafasi ya kwanza katika mitihani! |
Tumaini | Tamani ninyi nyote ni washindi! Mnastahili kupongezwa kwa kuwa mmeiletea sifa nzuri shule yetu. |
Nuru | Hapana! huwezi kulinganisha ushindi wa masomo na wa michezo! |
Amani | Ufaulu wa masomo, bila tabla nzuri ni kazi bure. |
Upendo | Msüdharau michezo kwani pia hujenga tabla nzuri. |
Tumaini | Sifa sio ufaulu wa masomo, michezo na tabla nzuri peke yake bali pia usafi. Tuipambe shule getu na kutunza mazingira. |
Amani | Ni kweli, ushindi wa kila mmoja wetu ni ushindiwa shule. |
Maswali
1. Je, ni mambo gani yanayoiletea sifa nzuri shule uliyojifunza kwenye majigambo uliyoyasoma?
2. Ni matendo gani zaidi unayoweza kutenda ili kuiletea sifa nzuri shule yako?
3. Te, unashiriki vipi katika shughuli mbalimbali za kuiletea sifa nzuri shule yako?
Kazi ya kufanya
Taja mambo yaliyowahi kuiletea sifa nzuri shule yako.
Msamiati
Kaulimbiu maneno au ujumbe unaohamasisha watu kutekeleza majukumu
Majigambo hali ya kutoa maneno ya kujisifia au kujikweza
Mazingira vitu vinavyotuzunguka katika eneo tunaloishi au kufanya kazi
Mpaka mahali panapotenganisha sehemu moja na nyingine
Nembo alama inayotambulisha kitu au sehemu kama vile shule na chama
Zoezi 1. Taja alama zilizomo katika nembo ya shule yako. 2. Andika matendo unayoyafanya kutunza mazingira ya shule yako. 3. Orodhesha vitu vinavyoitambulisha shule yako. 14. Orodhesha vitu vinavyopakana na shule yako. 5. Orodhesha mambo yanayofanyika shuleni kwako yanayokufanya uipende. |
www.learninghubtz.co.tz