STD VII HISABATI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MTIHAN1 LA TANZANIA

MTIHANI WA KUMALIZA ELIMIJ YA MSNGI

04 HISABATI

Muda: Saa 2:00 Mwaka : 2023

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
  2. Jibu maswali yote.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
  4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
  5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
  6. Weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali Ia 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
  1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
  2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali Ia 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi 45.

  3. Onesha wazi njia iliyotumika katika kujibu swali la 41 hadi 45 katika nafasi iliyotolewa kwenye fomu ya OMR.

  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: MATENDO YA KIHISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO

Katika swali la 1 - 40, kokotoa swali ulilopewa na kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Ni namba ipi inayofuata katika mpangilio wa namba zifuatazo? 29, 33, 37, 41,

  1. 43
  2. 45
  3. 47
  4. 42
  5. 46
Chagua Jibu


2. Urefu wa kiwanja cha mpira wa miguu ni meta 90.136 na urefu wa kiwanja cha mpira wa wavu ni meta 30.769. Andika tofauti ya urefu wa viwanja hivyo katika nafasi mbili za desimali.

  1. 60.63
  2. 59.34
  3. 60.37
  4. 59.37
  5. 59.36
Chagua Jibu


3. Akilimali alianguka baada ya kukimbia  ya muda wa saa moja. Je, ni asilimia ngapi ya muda alibakiza kukamilisha saa moja?

  1. 75%
  2. 0.25%
  3. 25%
  4. 7.5%
  5. 2.5%
Chagua Jibu


4. Bwana Mandela ana shamba lenye umbo la duara ambalo lina kipenyo cha meta 35. lwapo atapanda miti kwa achano la meta 2.2 kati ya mti na mti kuzunguka shamba hilo, je, atapanda miti mingapi kuzunguka shamba lote? (Tumia π =  )

  1. 110
  2. 242
  3. 77
  4. 51
  5. 50
Chagua Jibu


5. Daktari aliwahudumia wagonjwa kwa siku mbili. Siku ya Jumatatu aliwahudumia wagonjwa 81 na siku ya Jumanne aliwahudumia wagonjwa 69. Ipi ni sehemu ya wagonjwa waliohudumiwa siku ya Jumatatu?

Chagua Jibu


6. Rehema na Fadhili walianza kwa pamoja kuhesabu machungwa. Rehema alihesabu kwa sauti kila baada ya machungwa 5 na Fadhili kila baada ya machungwa 9. Ni namba ipi moja ya kwanza wote wataitaja kwa sauti?

  1. 14
  2. 4
  3. 45
  4. 90
  5. 54
Chagua Jibu


7. Tanki la pikipiki ya Bakari lilijazwa mafuta lita 24. Iwapo pikipiki itatembea umbali wa km 10 na kutumia  ya lita za mafuta hayo, je, ni lita ngapi za mafuta zitabaki?

  1. 15
  2. 34
  3. 9
  4. 25
  5. 14
Chagua Jibu


8. Basi lina viti 23, viti viwili ni kwa ajili ya dereva na kondakta na  ya viti vilivyobaki ni kwa ajili ya abiria. Ni viti vingapi havijakaliwa na abiria katika basi hilo?

  1. 21
  2. 14
  3. 16
  4. 7
  5. 9
Chagua Jibu


9. Wanafunzi watano walipewa kazi ya kuorodhesha vigawe vyote vya 6 vilivyopo kati ya 30 na 60. Ipi ni orodha sahihi?

  1. 36, 48,54, 56
  2. 36, 42, 54, 60
  3. 36, 40, 42, 48
  4. 36, 48, 54, 60
  5. 36, 42, 48, 54
Chagua Jibu


10. Esta alikokotoa kwa usahihi zao la namba tasa zote zilizopo kati ya 80 na 90. Je alipatajibu lipi?

  1. 7,387
  2. 7,378
  3. 7,367
  4. 7,373
  5. 7,396
Chagua Jibu


11. Makundi matano yaliorodhesha namba shufwa zote zilizopo kati ya 115 na 124. Kundi lipi liliorodhesha namba hizo kwa usahihi.

  1. 116, 120, 122, 124
  2. 116, 118, 120, 122
  3. 116, 119, 120, 122
  4. 116, 118, 120, 124
  5. 16, 120, 1239 124
Chagua Jibu


12. Wanafunzi walipewa kazi ya kupanga namba 1.25, 20%,  , 0.15 na -3 katika mfululizo wa kupungua. Upi ni mpangilio sahihi?

  1. 1.25,  , -3, 0.15, 20%

  2. -3, 1.25, 0.15, 20%,

  3. -3, 20%, 1.25,  , 0.15

  4. 1.25, 20%, 0.15,  , -3

  5. 1.25, -3, 20%, 0.15,

Chagua Jibu


13. Mwanahawa aliweka shilingi 450,000 kwa muda wa miaka 2 benki na kupata riba ya shilingi 27,000. Kipi ni kiasi cha riba kwa asilimia ambacho benki ilitoa.

  1. 2%
  2. 3%
  3. 4%
  4. 5%
  5. 1%
Chagua Jibu


14.Shule ya msingi Ushindi ina jumla ya wanafunzi 960. Ikiwa wasichana ni 540, je, wavulana ni sehemu gani ya wanafunzi wote?

Chagua Jibu


15. Mama yake Mariamu alikuwa na kilogramu 100 za mchele. Alimpa Elisha ,  Mwajuma  na Isihaka  ya kiasi chote cha mchele. Je, aliyepata mgao mdogo, alipata kilogramu ngapi za mchele?

  1. 30
  2. 40
  3. 70
  4. 20
  5. 10
Chagua Jibu


16. Musa alikula  ya mkate na Amina alikula  huo. Je, walibakiza sehemu gani ya mkate huo?

Chagua Jibu


17. Sabrina na Salma walipata faida katika biashara yao. Sabrina alipokea  ya faida wakati Salma alipokea 0.4 ya faida hiyo. Tafuta tofauti ya viwango walivyopokea katika asilimia.

  1. 60%
  2. 40%
  3. 30%
  4. 80%
  5. 20%
Chagua Jibu


18. Upendo alisafiri umbali wa kilometa  kwa baiskeli na sehemu iliyobaki alitembea kwa miguu. Iwapo alisafiri umbali wa kilometa  , je, alitembea umbali gani kwa miguu?

  1. Km

  2. Km

  3. Km

  4. Km

  5. Km

Chagua Jibu


19. Shule ya Msingi Uhuru ilikuwa na ng'ombe 80. Mwaka jana iliamua kuuza  ya ng'ombe hao. Je, shule ilibakiwa na ng'ombe wangapi?

  1. 50
  2. 48
  3. 32
  4. 10
  5. 30
Chagua Jibu


20. Kampuni ya umeme hutumia lita 5,500 na mililita 760 za dizeli kwa siku kufua umeme unaotosheleza katika kijiji cha Wazalendo. Ni kiasi gani cha dizeli kitatumika mwezi Februari wa mwaka mfupi kutosheleza mahitaji ya kijiji hicho?

  1. lita 154,021 na mililita 280
  2. lita 170,523 na mililita 560
  3. lita 165,022 na mililita 800
  4. lita 154,021 na mililita 250
  5. lita 159522 na mililita 40
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256