KISWAHILI STANDARD FOUR REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA IV TAREHE 23 NA 24 AGOST 2023

KISWAHILI

MUDA: SAA 1:30 AGOST 2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina jumla ya sehemu tano A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali 5
  2. Jibu maswali yote
  3. Andika majina yako kwa usahihi

SEHEMU A: IMLA

1. Sikiliza kwa umakini sentensi zinazosomwa kisha andika kwenye nafasi zilizo wazi.

i. image

ii. image

iii. image

iv. image

v. image

SEHEMU B:

2. Chagua herufi ya jibu sahihi

i. Kuku, bata, njiwa, kunguru na mwewe kwa jina moja huitwaje?

A: Wanaotaga B: Ndege C: Vikembe D: Wenye mabawa [     ]

ii. Mtu anayeongoza meli huitwa

A: Nahodha B: Rubani C: Dereva D: Mwalimu [     ]

iii. Ni neno lipi tutalipata tukidondosha herufi moja kwenye neno UJUZI?

A: Juzi B: Uzi C: Uuzi D: Juu [     ]

iv. Watoto watakula pilau kesho. Bainisha umoja wa sentensi hiyo

A: Watoto wanakula pilau B: Mtoto atakula pilau kesho

C: Mtoto wanapenda kula mapilau D: Mapilau yameliwa na watoto [     ]

v. Wanafunzi walifagia uwanja. Sentensi hii iko katika wakati gani?

A: Wakati ujao B: Wakati timilifu C: Wakati uliopo D: Wakati uliopita [     ]

SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

3. Tumia majibu yaliyoko kwenye kisanduku kujibu maswali yafuatayo.

Mchoyo, haina baraka, mlango, hajikwai, mafiga, hutunzwa

i. Tatu, tatu mpaka Tanga. Jibu la kitendawili hiki ni image

ii. Malizia methali hii. Mwenda pole image

iii. Kila mtu humwabudu apitapo image

iv. Andika maana ya Nahau hii. Ana mkono wa birika image


v. Malizia methali hii. Mcheza kwao image

SEHEMU D: UTUNGAJI

4. Panga sentensi zifuatazo kwa mfuatano sahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, D, na E ili kuunda habari sahihi

i. Rehema alimwambia mwalimu kuwa Hamidu anaumwa [     ] 

ii. Mwalimu Lupogo anafundisha somo la Sayansi [     ]

iii. Mwalimu alimgusa Hamidu akagundua ana joto kali [     ]

iv. Hamidu alipelekwa zahanati [     ]

v. Alipoingia darasani wanafunzi walisimama na kumsalimia [     ]

SEHEMU E: UFAHAMU

5. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa usahihi

Amina na Ali ni pacha. Wanaishi katika kijiji cha Kamachumu. Wote ni wanafunzi katika shule ya msingi Izigo. Kila siku huamka mapema na kujiandaa kwenda shuleni. Kabla ya kwenda shuleni, huwasalimia wazazi wao. Baada ya hapo, huagana nao na kuelekea shuleni. Wafikapo shuleni, huungana na wenzao kufanya usafi.

Kisha huingia darasdani na kuanza masomo. Watoto. Hawa wanapendwa na walimu wao kwa sababu ni watiifu.

MASWALI

i. Amina na Ali wanasoma shule gani? image

ii. Amina na Ali wanapendwa na walimu wao kwa sababu image

iii. Pacha waliotajwa kwenye habari hii ni image

iv. Amina na Ali wafikapo shuleni huungana na wenzao kufanya nini? image

v. Amina na Ali wanaishi katika kijiji gani? image

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

UPIMAJI WA UTAMILIFU MKOA DARASA LA NNE

 MKOA WA NJOMBE

01 KISWAHILI

Muda: Saa 1:30 Mwaka :2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina jumla ya maswali Matano (5) yenye sehemu A, B, C, D na E
  2. Jibu maswali yote.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Jina na Namba yako ya Upimaji katika sehemu ya juu kulia ya kila ukurasa.
KWA MATUMIZI YA UPIMAJI TU
 NAMBA YA SWALI   ALAMA   SAINI YA MPIMAJI
1

2

3

4

5

JUMLA

SAINI YA MHAKIKI


SEHEMU A: IMLA

1. sikiliza kwa makini sentensi zitakazosomwa kisha ziandike kwa usahihi.

i. __________________________________________________________

ii. ___________________________________________________________

iii. ___________________________________________________________

iv. ___________________________________________________________

v. ___________________________________________________________

SEHEMU B: MATUMIZI YA LUGHA:

2. chagua jibu sahihi na uandike herufi ya jibu sahihi.

i. Ninaomba_____________________________kwa kosa nililofanya

  1. Ladhi
  2. Radhi
  3. Razi
  4. Lazi [       ]

ii. Kinyume cha neno rejea ni:

  1. Rudia
  2. Nenda
  3. Rudi
  4. Subiria [       ]

iii. Baba aliniambia nimwandikie __________________ ya vitu ninavyohitaji kwa ajili ya shule.

  1. Orodha
  2. Orotha
  3. Oroza
  4. Olodha [       ]

iv. Kanusha sentensi hii “Mwanahamisi hula matunda”

  1. Mwanahamisi halagi matunda
  2. Mwanahamisi huwa hali matunda
  3. Mwanahamisi hali matunda
  4. Mwanahamisi hapendi matunda [       ]

v. Walimu huwa hawapendi kelele madarasani. Sentensi hii ipo katika hali gani? ________________________________

  1. hali timilifu
  2. hali ya mazoea
  3. wakati ujao
  4. wakati uliopita [       ]

SEHEMU C : METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

3. i. Wanafunzi wengi hawampendi mzee Kalinga kwa sababu ana mkono mrefu pia ana mkono wa birika. Kuwa na mkono wa birika ina maana gani?

____________________________________________

ii. Mwalimu alipoingia darasani aliandika maneno haya ubaoni. Tia moyo, Tia nanga, Piga marufuku na piga yowe. Kwa neno moja maneno haya yanaitwaje?

_______________________________________________

iii. Babu alituuliza vitendawili akasema ‘Jibu la kitendawili hiki ni lipi? “Nikimpiga mwanangu nalia mwenyewe’

_________________________________________

iv. Mimi ni mbwa ninapenda methali mbalimbali, ndondondo si chururu, fuata nyuki ule asali. Je, asiyesikia la mkuu  _______________________________________

v. Malizia methali isemayo ________________________________ hali wali mkavu.

SEHEMU D: UTUNGAJI

4. Panga sentensi hizi katika mtiririko ulio sahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E

i.

Mama yake aliporudi alifurahi sana.

[       ]

ii.

Aliosha vyombo na kufua nguo zake.

[       ]

iii.

Nguo zilipokauka alizianua na kuzinyoosha.

[       ]

iv.

Zawadi aliondoka kuelekea nyumbani kwao.

[       ]

v.

Kisha akaingia jikoni na kupika chakula.

[       ]

SEHEMU E: UFAHAMU

5. Soma habari kisha jibu maswali

Nyumbani kwetu tupo watoto watatu tu, mtoto wa kwanza ni mimi Aisha ninasoma darasa la saba. Mtoto wa pili ni Hamisi ambaye anasoma darasa la tano. Anayemfuata Hamisi anaitwa Juma ana umri wa miaka mitano, yeye anasoma darasa la awali.

Baba na mama ni wakulima hodari wanalima mazao mbalimbali pamoja na kilimo wanafanya kazi zingine kwa bidii. Baba na mama wanatusisitiza tufanye kazi kwa bidii hawataki mtu mvivu. Pia wazazi wanatusisitiza kufanya bidii katika masomo ili tuwe na maisha bora hapo baadaye.

MASWALI.

i. Baba na Mama ni _____________________________________ hodari.

  1. Wafugaji
  2. Wakulima
  3. Wafagizi
  4. Walimu [       ]

ii. Ili uwe na maisha bora hapo baadaye inakupasa?____________

  1. Kuwa mvivu
  2. Kuwa mzurulaji
  3. Kusoma kwa bidii
  4. Kucheza kamali [       ]

iii. Kifungua mimba ni____________________________________

  1. Aisha
  2. Hamisi
  3. Juma
  4. Baba [       ]

iv. Mziwanda ana umri wa miaka mingapi?____________________

  1. Mitatu
  2. Minne
  3. Miwili
  4. Mitano [       ]

v. Nyumbani kwa Aisha kuna jumla ya watu wangapi?__________

  1. Watatu
  2. Watano
  3. Wanne
  4. Wawili [       ]


STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 22  

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 22  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM


UPIMAJI WA UTAMILIFU WA KATA DARASA LA IV - 2023

KISWAHILI [01]

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali matano (5)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu
  3. Majibu yote yaandikwe kwa herufi kubwa isipokuwa Imla.
  4. Tumia kalamu ya wino wa rangi ya bluu au mweusi
  5. Simu za mikononi na vifaa vingine visivyohitajika haviruhusiwi katika chumba cha
    mtihani.

JINA LA MTAHINIWA: _____________________________________
JINA LA SHULE: _______________________________________
WILAYA: ____________________MKOA:__________________

Muda: Saa 1:30 Julai , 2023

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU
NAMBA YA SWALI ALAMA   JINA LA MTAHINI
1.
2.
3.
4.
5.
JUMLA
SAINI YA MWINGIZA 
SAINI YA MHAKIKI

SEHEMU A: IMLA 
1. Sikiliza kwa umakini sentensi utakazosomewa na uziandike kwa usahihi.

i. ___________________________________________________________

ii. ___________________________________________________________

iii. ___________________________________________________________

iv. ___________________________________________________________

v. ___________________________________________________________

SEHEMU B: SARUFI NA MSAMIATI
2. Chagua jibu sahihi kisha uandike herufi kwenye parandesi 
 ulizopewa.
i. Uwanja wa ndege wa Tanzania ni mzuri sana. Wingi wa neno uwanja ni_____
A. Mauwanja B. Wanja
C. Nyanja D. Viwanja [ ]

ii. Orodha ipi ya maneno inajumuisha wadudu kati ya hizi?
A. Mawio, machweo, zama, kunguni B. Kupe, chawa, kunguru, papasi
C. Suruali, gauni, nyigu, mchwa D. Kupe, papasi, chawa, kunguni [ ]

iii. Kwangu anapenda sana usafi, mtu mwenye tabia ya kuwa safi daima huitwa?
A. Mweupe B. Mzuri
C. Mtanashati D. Mfagiaji [ ]

iv. Shangazi amemkodolea macho utingo. Ukanushi wa sentensi hii ni upi?
A. Shangazi hajamkodolea macho utingo
B. Shangazi hamkodolei macho utingo
C. Shangazi humkodolea macho utingo
D. Shangazi huwa hamkodoleagi macho utingo [ ]

v. Mbwa wetu mweusi si mkali. Kinyume cha neno mkali ni;
A. Mweupe B. Mwizi
C. Mkaidi D. Mpole [ ]

SEHEMU C: LUGHA ZA KIFASIHI

3. METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
i. Nahau mkono wa birika ina maana gani?
____________________________________________________________

ii. Kamilisha methali hii hakuna masika ______________________________

iii. Kabudi alipokea chakula alichopewa na mama yake kwa shingo upande.
Nahau shingo upande ina maana gani? ____________________________

iv. Nina chemchemi isiyokauka. Jawabu la kitendawili hiki ni
____________________________________________________________

v. _______________________________ si dawa ya pengo. Maneno yapi ni
mwanzo mzuri wa methali hiyo?

SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Tumia maneno yafuatayo kujaza katika nafasi zilizoachwa wazi.
 Epua, kuchemka, upishi, vifaa, viungo

Mwalimu wetu wa somo la Sayansi alieleza hatua za kuandaa chai kama ifuatavyo;
Tulijifunza kuchemsha chai ya rangi kwa kutumia jiko la gesi. 

Andaa 

(i) ________vyote vinavyohitajika katika 

(ii) _________________ wa chai. Weka sufuria yenye maji kwenye jiko lililowashwa. Weka tangawizi na 

(iii) _______________________ vingine kama utapenda. Maji yanapokaribia

 (iv)____________________________ weka majani ya chai na uiache ichemke kwa muda.

 (v) _____________________, Chai yetu iko tayari kunywewa.

SEHEMU E: UFAHAMU
 5. Soma Habari ifuatayo kisha jibu maswali

Ilikuwa ni wakati wa usiku. Siku hiyo kulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na radi. Nilikuwa chumbani kwangu nikisoma kitabu cha hadithi. Mara nilimsikia baba akiniita Mboni! Mboni! zima taa ulale kuna radi sana. Baada ya muda mfupi nikalala fofofo na kuota ndoto nzuri sana. Niliota tumekwenda Zanzibar kutembelea makumbusho tulipokuwa huko tulikwenda Forodhani kuona jumba la mfalme. Tulipoingia ndani tukaona vitu mbalimbali vya kale. Tuliona vitu kama mapanga, sarafu, mbuzi za kukunia nazi na majiko ya asili. Pia tuliona samani na vitanda vyenye besera na magodoro ya sufi. Siamini macho yangu natamani ndoto yangu irudie!

MASWALI

i. Nani aliota ndoto nzuri baada ya kulala fofofo?
______________________________________________________________

ii. Kwanini baba yake alimwambia azime taa?
_____________________________________________________________

iii. Nahau lala fofofo kama ilivyotumika kwenye habari ina maana gani?
_____________________________________________________________

iv. Nyumba anayoishi mfalme huitwaje? _______________________________

v. Neno besera kama lilivyotumika katika habari hii lina maana gani?
_____________________________________________________________

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 13  

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 13  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA NNE

KISWAHILI

SEHEMU A:IMLA

1.Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa kisha ziandike kwa usahihi

(i)……………………………………………………………

(ii)………………………………………………………………

(iii)……………………………………………………………..

(iv)…………………………………………………………….

(v)……………………………………………………………..

SEHEMU B:MATUMIZI YA LUGHA

2.Chagua jibu sahihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye kisanduku ulichopewa

(i)Mtoto mwenye adabu ………………..

(A)Hulia hovyo(B)Hupendwa na watu wengi(C)Huosha hovyo(D)Hupigwa na walimu (     )

(ii)Mama alinunua hereni za ………………………..

(A)Dhahabu(B)Zahabu(C)Dhaabu(D)Zaabu(     )

(iii)Majira yapi huwa na mvua za rasharasha? 

(A)Masika(B)Kiangazi(C)Kipupwe (C)VVuli (     )

(iv)………………..ni mtu anayeendesha meli.

(A)Mahiri(B)Dereva(C)Nahodha (D)Rubani (     )

(v).Binamu ni motto wa …………

(A)Babu(B)Mjomba(C)Dada(D)Kaka (     )

SEHEMU C : METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

3.Kamilisha kazi za kifasihi zifuatazo kwa kuandika jibu sahihi kwa kila swali.

Kamilisha methali zifuatazo

(i)Usipoziba ufa …………………….

(ii)Kuishi kwingi……………………..

(iii)Nini maana ya nahau “amevaa miwani”………………………

(iv)Tegua kitendawili kifuatacho.”mjoma hataki tuonane”

(v)Kuvunjika moyo maana ake ni ……................................

SEHEMU D:UTUNGAJI

4.Chagua maneno kutoka kwenye kisanduku kukamilisha habari

Zangu,jokofu,ndoto,thamani,pangaboi

Siku moja niliota ndoto(i)………….nzuri sana.Niliota nikiwa kwenye jumba kubwa zuri lenye kila kitu cha(ii)………….Kulikuwa na viyoyozi vilivyoleta hewa nzuri mno(iii)……….lilijaa vinywaji na matunda.Ghafla nilistuka na kukuta(iv)………likiendelea kuzunguka juu ya dari na siye kiyoyozi.Sikuwasimulia rafiki(v)……………ile ndoto kwani wangeishia kunicheka.

SEHEMU E:UFAHAMU

5.Soma shairi kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo

Pata ung’oapo jino,uwazi unabakiza

Sura ya huzuni mno,tena ya kufurahia

Nataka unga mkono,penye nia pana njia

Ishirini moja tano,maua yangu chanua

MASWALI

(i)Shairi hili lina beti?..............

(ii)Neno huzuni ni kisawe cha neno gani?...............

(iii)Andika kituo cha hili………………………………………….

(iv)Unapong’oa jino kuna baki nini…………………………

(v)Ubeti huu una mishororo mingapi……………………..

 

IMLA

(i)Mama anakula ugali na dagaa

(ii)Shuleni kwetu kuna maua

(iii)Baba na mama ni wafanyakazi

(iv)Nitaenda shuleni jumatatu

(v)Nitaimba wimbo


STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 8  

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 8  

Jina la Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Namba ya Upimaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI

MTIHANI WA UJIPIMAJI WA WILAYA DARASA LA NNE

 01 KISWAHILI

Muda:SaaI: 45 Septemba, 2022

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E zenye jumla ya maswali matano (05)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkon( na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha taji.
  6. Andika Jina Namba ya Upimaji seherntı yajuu kulia katika kila ukurasa.

KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAINI YA MPIMAJI

1.



2



3



4



5



JUMLA



SAINI YA MHAKIKI


SEHEMU A(A1ama 10) 

IMLA

1. Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa na msimamizi wa mtihani kisha uziandike kwa usahihi.

  1.  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  2.  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  3. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  4. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  5. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

SEHEMU B

(Alama 10)

2. Chagua herufi yajibu sahihi na uiandike katika kisanduku ulichopewa

(i). Mtu anayeongoza meli na kuifikisha mahali inapohitajika huitwa

  1. Rubani
  2. Dereva
  3. Nahodha 
  4. dereva wa meli

(ii) Sentensi hii ipo katika wakati gani? "Mtoto hakula chakula"

  1. Mazoea
  2. Timilifu
  3. Uliopita 
  4. Ujao 

(iii). "Chungu cha shangazi yangu ni kizuri" wingi wa sentensi hii ni..

  1. Vyungu vya shangazi yangu ni vizuri
  2. Vyungu vya shangazi zetu ni vizuri
  3. Vyungu vya mashangazi wetu ni vizuri
  4. Vyungu vya washangazi wangu ni vizuri

(iv) Taja neno moja linalo beba maneno haya, mfenesi, mpera, mkomamanga, mpapai. 

  1. Matunda 
  2. Mimea
  3. Mazao 
  4. Viungo

(v) Neno "shaghalabaghala" lina silabi ngapP

  1. Nne 
  2. Tatu
  3. kumi na tano 
  4. Sita

SEHEMU C (Alama 10)

3. Andika jibu sahihi kwa maswali yafuatayo:

(i). Andika methali inayofanana na "Jungu kuu halikosi ukoko."

(ii) Utatumia methali gani kumuonya mtu anayependa kuuliza sana maswali ili kuelewajambo?

(iii) Nini maana ya methali "Haba na haba hujaza kibaba?"

(iv) Baada ya kikao cha familia na wana ukoo tulimaliza msiba na kuanza safari. Ni nahau gani inafaa kwa maelezo haya?

(v) Ni kitendawili gani ambacho jibu lake ni MBARIKA?

4. Andika sentensi zifuatazo kwa usahihi. Hakikisha unaweka alama sahihi za uandishi na herufi kubwa. 

(i) atu anaishi mkoa wa arusha

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(ii). wanafunzi walitembelea mbuga za wanyama za mikumi manyara, na tarangire

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iii) lo mtoto ameanguka

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iv). shambani kwa babu kuna mazao gani

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(v). shangazi alisema karibu mpwa wangu

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

SEHEMU E (Alama10)

UFAHAMU

5. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

Siku ya Jumatatu, Imani aliamka asubuhi na mapema kwenda shuleni. Njiani alikuta ajali ya mtu aliyeanguka na baiskeli. Alipoangalia kando ya barabara, alimuona mtu amelala chini. Alipoangalia pembeni yake, aliona tenga la nyanya na baiskeli. Usukani na gurudumu la mbele la baiskeli vilikuwa vimepinda. Baadhi ya nyanya zilizokuwa kwenye tenga nyingine zilikuwa zimesambaa barabarani. Imani alimuuliza kijana aliyeitwa Bakari, "Kaka kumetokea nini hapa?"

Yule kijana akamjibu. "Kumetokea ajali, mwendesha baiskeli nmeteleza na kuanguka" Imani alisikitika sana. Akauliza tena, "Je, ameumia?" Yule kijana akamjibu, "Sina uhakika ila amepoteza fahamu". Imani akauliza tena, "Mbona hamumpeleki hospitali?" yule kijana akajibu, "Ajali imetokea sasa hivi"

Imani aliendelea na safari ya kuelekea shuleni. Mbele kidogo alikutana na mwendesha pikipiki. Alimsimamisha na kumwueleza kuhusu mwendesha baiskeli aliyepata ajali. Akamuomba kama anaweza kwenda kumsaidia. Yule mwendesha pikipiki alikubali kwenda kumchukua na kumpeleka hospitali.

MASWALI

(i). Nani aliamka mapema kwenda shuleni

(ii). Ajali iliyotokea barabarani ilikuwa ni ya nini?

(iii). Nani aliulizwa na Imani kuhusu kilichotokea

(iv). Je. Imani ni mwanafunzi mwenye tabia gani

(v). Nani aliyemsaidia mwendesha baiskeli na kumpeleka hospitali

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 6  

STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 6  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256