?> KISWAHILI STANDARD SEVEN EXAMS SERIES
KISWAHILI STANDARD SEVEN EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UMAHIRI KWA SHULE ZA MSINGI

UPIMAJI DARASA LA SABA MTIHANI WA MWIGO

KISWAHILI

2024

 

MUDA: 1:30                                                                                                         

MAELEKEZO 

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali Sita (6) 

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu 

3. Majibu yote yaandikwe katika karatasi hii 

4. Tumia kalamu ya wino wa rangi ya bluu au mweusi 

5. Simu za mikononi na vifaa vingine visivyohitajika haviruhusiwi katika chumba cha mtihani. 

6. Andika kwa usahihi :Jina lako na Jina la Shule kwenye sehemu ulizopewa. 

SEHEMU A: (Alama 20)

1. Sikiliza kwa makini hadithi itakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la i- v kwa kuandika herufi ya jibu iililo sahihi kwenye mabano. 

i) Sifa za mwalimu zilivuma maana yake? (a) sifa zilipeperushwa (b) sifa zilisikika bara zima la Afrika (c) sifa zake zilisikika na kuenea pote   (d) sifa za mwalimu zilisambaa Tanzania nzima (e) mwalimu alifahamika sana 

ii) Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa watu gani barani Afrika? (a) watu makini (b) watu wakubwa (c) watu walemavu (d) watu mashuhuri (e) watu walevi 

iii) Hekima na busara za Mwalimu Nyerere zilioneshwa katika (a) hotuba zake (b) umri wake (c) watu wakubwa (d) umaarufu wake (e) uongozi wake 

iv) Hotuba za Mwalimu Nyerere zilikuwa na mpangiko mzuri wa (a) maneno (b) lugha (c) utaratibu (d) matamshi (e) falsafa 

v) Mwalimu Nyerere alikuza, aliendeleza na kuimarisha (a) lugha ya Taifa (b) mitaala  (c) kiswahili (d) kingereza (e) muhtasari 

 

2. Chagua jibu lililo sahihi kutoka katika machaguo uliyopewa, kisha andika parandesi ulizopewa

  1.        Mjomba amekwenda kumuona bibi. Neno lipi limetumika kama kielezi katika sentensi hii? (a) Bibi (b) Kijiji (c) Amekwenda (d) Mjomba (e) Kumuona
  2.       Baba, mama, mimi na wadogo zangu tunapenda kula ugali. Sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi? (a) Ya tatu umoja (b) Ya tatu wingi (c) Ya pili umoja (d) Ya kwanza wingi (e) Ya kwanza umoja
  3.     Humo------------ alimoingia yule nyoka. Neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?

(a)Ndiye (b) Ndiko (c) Ndipo (d) Ndio (e) Ndimo 

  1.    Neno lipi ni tofauti na mengine kati ya haya yafuatayo? (a) Mpasuko (b) Mshikamano (c) Ushirikiano (d) Umoja (e) Muungano
  2.       "Jana asubuhi walisoma kitabu cha hadithi" Kiambishi cha njeo ni kipi? (a) Wa- (b) Li- (c) -soma-(d) -a (e) -Ii-
  3.    Mfuko umechanika vibaya, neno lililopigiwa mstari lipo katika ngeli gani? (a) KI-VI (b) LI-YA (c) I-ZI (d) A-WA. (e) U-1
  4.  Neno bughudha lina silabi ngapi? (a) Tatu (b) Mbili (c) Nne (d) Sita (e) Nane
  5.            Mtu mwenye taaluma ya ujuzi wa kubuni kutengeza au kurekebisha barabara, au mitambo anaitwa nani? (a) Rubani (b) Dereva(c) Mkutubi  (d) Mhandisi (e) Mhunzi

ix) Vifuatavyo ni vipengele vya barua ya kirafiki, isipokuwa  (a) Anuani ya mwandishi (b) Tarehe (c) Anuani ya mwandikiwa (d) Mwanzo wa barua (e) Jina la mwandishi 

 x) Maneno yafuatayo yameandikwa kwa kirefu, fupisha maneno Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. . (a) Teknolojia (b) Habari (c) TMH (d) Mawasiliano (e) Tehama 

3. Oanisha maneno ya sehemu A na maana yake katika sehemu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye nafasi uliyopewa 

SEHEMU A

SEHEMU B

  1. Mofa
  2. Kiini
  3. Saladi
  4. Mafya
  5. Mseto
  1.               Chanzo, sababu au undani wa jambo, kisa au tukio
  2.               Mafiga
  3.               Mvurugano wa mambo hali ya vurugu, ugomvi au sokomoko
  4.              Mchanganyiko wa vitu au mambo mbalimbali
  5.                Mkate uliotengenezwa kwa unga wa nafaka
  6.                Mchanganyiko wa mboga au matunda unaoliwa bila kupikwa

 

4. Panga sentensi zifuatazo ili zilete mtiririko unaofaa kwa kuziandika upya

i) Waliamini kuwa mtu anayeugua Ukimwi amelogwa 

ii) Hivi sasa ugonjwa huu unafahamika na kila mtu anachukua tahadhari

  1.                 Wengi wao walihusisha ugonjwa huu na imani za kishirikiana
  2.                   Zamani watu wengi hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya ugonjwa wa Ukimwi
  3.                 Hivyo walihangaika mchana na usiku kutafuta waganga wa kienyeji

5. Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata. 

Kidato nimemaliza, tangu ule mwaka juzi, 

Maswali nimemaliza, kwa walimu na wajuzi, 

Mingi pia nimecheza, michezo kwao juzi, 

Sanaa nayo elimu, shuleni sikutegea 

Najionea fahari, kuitwa mtaalamu, 

Napata nyingi safari, kwa wangu utaalamu, 

Sitochoka kukariri, nilopata kwa walimu,

 Elimu kitu muhimu, usilaumu walimu. 

Utaukosa uhondo, neema tele na raha, 

Kumbukizi la mikondo, sikuliona fedheha,

 Nyota pia na vimondo, havikunipa jeuri, 

Elimu nguzo muhimu, pata ukajionee 

MASWALI. 

i) Shairi ulilosoma lina jumla ya beti kamilifu ngapi?   

ii) Neno "fedheha" kama lilivyotumika katika ubeti wa tatu lina maana gani? 

iii) Kwa kuzingatia sifa Ea mashairi, shairi hili ni aina gani ya shairi? 

iv) Andika vina vya kati na mwisho katika ubeti wa pill  na  

 v) Kituo katika ubeti wa tatu kina mizani ngapi?  

SEHEMU C: 

6. Kamilisha barua ifuatayo kwa kutumia maneno yaliyopo kwenye kisanduku. 

Andika majibu sahihi katika sehemu wazi 

i. Mbwa wetu ni mkali sana. neno lilopigiwa mstari ni aina gani ya maneno? ________________________ 

ii. Nini jibu la kitendawili hiki? “Chungu cha mwitu hakipiki wapishi wake wakaiva.” ___________________ 

iii. Nitasoma sana ili nifaulu mtihani wangu. Sentensi hii ipo katika nafsi ipi? ________________________ 

iv. Mwanafunzi aliyechelewa shuleni amefukuzwa. Hii ni aina gani ya tungo? ________________________ 

v.Je, kamusi ina sehemu kuu ngapi? _______________________________

 

Habari isomwe na msimamizi kwa kuzingatia kanuni za usomaji. Maelekezo kwa msimamizi 

(i) Uwaruhusu wangfunzi wasikilize lava umakini 

(ii) Soma habari kwa umakini. 

(iii) Wanafunzi hawaruhusiwi kujibu maswali wakati unasoma habari. 

(iv) Soma habari mara mbili, kisha waruhusu wajibu maswali i-v. 

Hayati Mwalimu Nyerere ni miongoni mwa watu mashuhuri Barani Afrika. Popote alipotembea sifa zake zilivuma kwa wingi wa heshima na busara zake zilizojidhihirisha katika hotuba zake alizowahi kutoa. Alitumia Kiswahili fasaha bila ya kuingiza maneno ya lugha kutoka Ughaibuni. Mamia na maelfu ya Watanzania walipenda kusikiliza hotuba zake kwa hamu kubwa bila ya kuchoka na mpangilio mzuri wa lugha ya Kiswahili aliyoitumia mara nyingi kuhutubia Taifa. Zaidi ya hayo, Hayati Mwalimu Nyerere hatasahaulika kwa kipaji cha kukuza, kuendeleza na kuimarisha Kiswahili. Kama ilivyo ada kwa watanzania wote kuendeleza Kiswahili.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 103

MTIHANI WA MAJARIBIO DARASA LA SABA-MUUNDO MPYA

SOMO: KISWAHILI 

MACHI 2024 MUDA: SAA1:40

MAELEKEZO:

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye maswali 6 yenye jumla ya vipengele 35.
  2. Tumia kalamu ya wino mweusi au bluu kujibia mtihani.
  3. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo katika kila kipengele.
  4. Zingatia usafi na mpangilio mzuri katika kazi yako.
  5.  Simu, vishikwambi na saa janja haviruhusiwi kwenye chumba cha mtihani.

 

SEHEMU: A (alama 20) 

  1. Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi kisha jibu maswali yafuatayo kwa kuchagua herufi ya jibu lililo sahihi. (alama 5)
  1. Katika sherehe ziliundwa kamati mbalimbali ili kufanikisha sherehe hiyo. Kamati ya mazingira alihudumu nani? A. Panya B. Bundi C. Kipepeo D. Mjusi E. Nyuki [ ]
  2. Wanakamati wote walikuwa wanapatikana katika eneo wanaloishi lijulikanalo kama  A. Ukumbini B. Kwenye sherehe C. Harusini D.Darini E. Kamati [ ]
  3. Paka ,Panya, Bundi na Mjusi wote walikuwa katika kamati lakini chini ya uongozi wa nani kati yao? A. Paka B. Bundi C. Panya D. Mjusi E. Kipepeo [ ]
  4. Ukumbi ulipambwa kwa maua, nakshi na vito mbalimbali. Vito hutengenezwa kwa kutumia A. Maua B. Mapambo C. Madini D. Taa za rangi E. Urembo Urembo [ ]
  5. Wanakijiji walikuwa na shauku ya sherehe ya mwaka. Hii ilipelekea kuwa na maandalizi kabambe. Neno shauku limetumika likiwa na maana ya  A Pilikapilika B. Mshawasha C. Tahayari D. Kabambe E. Furaha [ ]
  1. Chagua na uandike herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya kujibia. (alama 10)
  1. Matilda ni msichana mrembo. Urembo wake unawavutia watu wengi. Neno "Urembo" limetumika kama aina ipi ya neno? A. Kivumishi B. Kiwakilishi C. Kishirikishi D. Sifa E. Nomino. [ ]
  2. Maneno hufanana na hutofautiana kimaana. Je, neno lipi ni tofauti na mengine katika orodha ifuatayo? A Hondohondo B. Kwereakwerea C. Mkunguru D. Mumbi E. Tausi [ ]
  3. Hayati Lowasa aliwahi kusema "kutekeleza jambo kunahitaji vitendo, Tusiridhike na kutoa maelekezo tu. Maneno haya yanasadifiwa na methali ipi kati ya hizi? A. Mpanda hila huvuna ufukara B. Jumbe ni watu si kilemba C Mazoea huleta dharau D. Maagizo matupu hayahimizi kazi E Mvuvi ndiye ajuaye pweza alipo [ ]
  4. .Mwalimu alifoka kwa jazba na kusema , Kwanini mnachelewa kufika shuleni? "Je, sentensi hii ipo katika kauli ipi? A. Tata B. Halisi C. Taarifa D. Mazoea E. Isiyoeleweka
  5. Baba alituonya baada ya kuchelewa kurudi nyumbani kuwa mtu anapohusiana na mtu mbaya, huishia kuambukizwa ubaya huo. Methali ipi inashabihiana na maelezo ya baba? A. Haba na haba hujaza kibaba B. Mcheza na tope humrukia C. Kalamu mbili zilimshinda fisi D. Kiingiacho mdomoni si haramu E. Tabibu hazuii ajali [ ]
  6. ."Mtaamua kufagia au mtapiga deki?" Aliuliza Topasi. Je, sentensi hii iko katika nafsi ya ngapi? A. Wingi sana B. Pili wingi C. Tatu wingi D. Kwanza wingi E. Tatu umoja. [ ]
  7. Hapa utakapojengwa mnara mkubwa kwa ajili ya azimio la Elimu kwa vitendo. Neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi? A. Ndiyo B. Ndo C. Ndiko D. Ndipo E. Ndimo [ ]
  8. Alifika kijijini na kuwajengea nyumba nzuri wazazi wake. Neno "kuwajengea" lipo katika kauli gani? A. kutenda B. kutendea C. Kutendeka D. Kutendwa E . Kutendeana [ ]
  9. Serikali imeendelea kuwashika mkono makundi mbalimbali ili yaweze kujikwamua kiuchumi. Shika mkono ina maana ya _____ A. Enda pamoja B. karibia C. Ongoza D. Toa msaada E. Fuatilia [ ]
  10. Mkuu wa mkoa ameendelea kuhimiza wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kuepuka la Ebola A. ugonjwa B bala C. baa D. shida E maambukizi [ ]
  1. Oanisha Sehemu A na sehemu B ili kukamilisha maana kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kutoka kifungu B katika sehemu ya kujibia. (alama 5)

SEHEMU: B (alama 20) 4.

Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili zilete mtiririko mzuri. (alama 10) 

  1. Wanyama pori ni nyara za serikali [ ]
  2. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kulinda rasilimali hii [ ]
  3. Msasi mmoja huuza meno hayo kwa wafanyabiashara waovu [ ]
  4. Ndovu ni miongoni mwa wanyama pori maarufu [ ]
  5. Watu wengi wamewaua tembo na kuchukua meno yao [ ]

 

5. Soma habari ifuatayo kwa umakini kisha jibu maswali yanayofuata (alama 10) Kenebegi alichukua rununu ya mama yake akiwa na nia ya kutafuta michezo mbalimbali. Akiwa katika kutafuta njia ya kuweza kuingiza nywila mara kadhaa bila mafanikio, Mama yake alimkuta na kustaajabu huku akiuliza "Ni nani kakuruhusu kuchezea rununu yangu?". Rununu hii ndio chanzo cha mapato kwa kufanya huduma mbalimbali, si vema kuichezea bila kibali changu. Kenebegi Mponjoli alimwangukia mama yake na kuahidi hatorudia tena. 

MASWALI 

  1. Baba yake na Kenebegi aliitwa nani? 
  2. Kenebegi alishindwa kuingiza nywila na kuendelea na matumizi. Neno nywila lina maana ya 
  3. Mama yake Kenebegi hutumia rununu kama nini?
  4. Rununu ni Kisawe cha
  5. Habari hii ina aya ngapi? 

SEHEMU: C (alama 10) 

6.Andika mambo matano yaliyokosekana katika barua hii

Afisa Kilimo wa Wilaya, (i)  Mvomero 3/04/2022 

(ii)  (iii)  Ndugu, YAH: KUPOKEA MBOLEA  Tafadhari rejea mada tajwa hapo juu. Tumefanikiwa kupokea mbolea mifuko 300 (mia tatu) Wakulima wamefanikiwa kupata mifuko ya mbolea kwa wakati na watafuata maelekezo ya wataalamu. Tunashukuru kwa ushirikiano (iv)  (v)  

 

 

HABARI 

Siku moja katika kijiji cha Darini kulikuwa na pilikapilika za hapa na pale. Wanakijiji walikuwa na shauku ya sherehe ya mwaka. Shauku ilichochewa na maandalizi kabambe yaliyofanywa kwa kuunda kamati mbalimbali. Kiongozi mkuu aliitwa bundi, alimteua Paka mkuu wa kamati ya vinywaji, Panya alipewa kazi ya kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi. Mjusi alikuwa muandaaji wa vyakula vya sherehe. Kamati ya mapambo iliyokuwa chini ya uongozi wa kipepeo iliupamba ukumbi kwa maua, nakshi na vito mbalimbali. Kila aliyefika ukumbini aligawiwa vinywaji avipendavyo na chakula akitakacho Ama kweli sherehe ilifana.

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 93

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

JARIBIO LA KUJIPIMA NUSU MUHULA WA KWANZA 2024 

                         SOMO: KISWAHILI DARASA: VII 

SEHEMU A (ALAMA 20) 

  1. Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa na msimamizi wako kisha jibu kipengele cha i-v kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi
  1. Kwa mujibu wa habari uliyosikiliza nini maana ya maisha? A. Maisha ni silaha B. Maisha ni vita C. Maisha ni uhai D. Maisha ni kuishi E. Maisha ni kusoma [ ]
  2. Kwanini mwanafunzi upo shuleni? A. ili kupambana B. ili kunoa silaha C. ili ukue vyema D. ili uweze kujua maana ya maisha E. ili kucheza na wenzako [ ]
  3. Ni wapi mtu huweza kujifunza maana ya maisha? A. shuleni B. chuoni C. hakuna sehemu yoyote D. chuoni na shuleni E. kanisani [ ]
  4. Ikiwa mtu anatamani kuwa na nyumba,gari au mali yampasa kufanya nini? A. kuishi B. kwenda shule C. kuhamia mjini D. kuanzisha biashara E. kupambana [ ]
  5. Kwanini mnasisitizwa kutumia vyema muda wenu muwapo shuleni? A. ili kufaulu vyema B. ili kuepuka maisha C. ili kuyashinda maisha D. ili kutojuta baadaye E. ili kukua vyema
  1. Chagua jibu sahihi na kisha uandike herufi ya jibu sahihi hilo katika sehemu ya kujibia.
  1. Walifanya kazi ile bega kwa bega hadi ilipokamilika. Nahau “bega kwa bega” inafafanuliwa na kifungu kipi cha maneno? A. kujituma sana B. walishirikiana kwa pamoja C. walitumia nguvu nyingi D. walifanya kwa uzalendo E. walitumia maarifa sana [ ]
  2. Nahau ipi yenye maana ya “kuzama au kuogelea majini?” A. piga maji B. zama maji C. piga mbizi D. piga kumbo E. piga zengwe [ ]
  3. “Utakapowasili hapa utahutubia wananchi”. Mzungumzaji ametumia nafsi gani kati ya hizi? A. nafsi ya pili umoja B. nafsi ya kwanza wingi C. nafsi ya kwanza umoja D. nafsi ya tatu umoja E. nafsi ya tatu wingi [ ]
  4.  “Yanga wamefuzu katika hatua ya mtoano”. Kauli hiyo inawakilisha nafsi ipi kati ya hizi zifuatazo? A. nafsi ya kwanza wingi B. nafsi ya pili wingi C. nafsi ya kwanza umoja D. nafsi ya tatu umoja E. nafsi ya tatu wingi [ ]
  5. “Aminata amefaulu mtihani”, mwalimu alisema. Hiyo ni aina gani ya kauli kati ya hizi zifuatazo? A. mazoezi B. halisi C. tata D. taarifa E. tendwa [ ]
  6.  “Juma anasoma ingawa Neema anacheza”. Neno “ingawa” ni aina gani ya neno? A. kitenzi B. kihisishi C. kiiunganishi D. kielezi E. kiwakilishi [ ]
  7. Rehema _____mama yake Mary. Neno linalokamilisha sentensi hii ni lipi? A. siyo B. sio C. sie D. siye E. si [ ]
  8. Hapa ____alipozikwa hayati Ali Hassan Mwinyi. A. ndiko B. ndimo C. nipo D. ndipo E. ndicho [ ]
  9.  “Sitakubali kuondoka”. Neno “sitakubali” liko katika hali gani? A. ukanushi B. mazoea C. timilifu D. endelevu E. halisi [ ]
  10.  “Damu ni nzito kuliko maji”. Methali hii inahusiana na ipi kati ya hizi zifuatazo? A. mchumia juani hulia kivulini B. penye nia pana njia C. mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe D. mbio za sakafuni huishia ukingoni E. baada ya dhiki faraja [ ]

3. Katika sehemu hii oanisha methali zinazofanana kutoka sehemu A na B kwa kuandika herufi va jibu sahihi 

 

SEHEMU B (ALAMA 20) 

4. Katika sehemu hii kamilisha sentensi kadri ulivyoulizwa kwenye kipengele husika 

  1. Meza, kabati, kiti na kitanda kwa neno moja huitwaje? 
  2. Abdalah alitapanya mali za urithi. Kinyume cha neno tapanya ni nini? 
  3. 3. Kazi ya Amina ni kijungujiko. Kazi ya kijungujiko ni kazi ya aina ipi? 
  4. Kitoto hiki kinacheza kitoto. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina ipi ya maneno?
  5. Nashon hufanya kazi ya kuhifadhi na kuazimisha vitabu kwa wasomaji katika maktaba ya mkoa. Je, Nashon ni nani? 

5. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata 

Kaitwa mahakamani, popo kujibu shitaka, 

Hakimu naye makini, hadhira shauku tua, 

Atakiwa abaini, kwa ulimi kutamka, 

Ajitetee bayana, ni mnyama au ndege 

Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea, 

Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea, 

Sina jadi na kunguru, ila na pundamilia, 

Mimi ni mnyama huru, amini ninakwambia, 

Tukidaiwa ushuru, kwa Wanyama nalipia. 

Ni kweli popo napaa, na mabawa nimepata, 

Lakini mimi nazaa, hilo halina utata, 

Nazaa na kunyonyesha, sina undugu na bata 

Wale wanaopotosha , niwaonyeshe matiti. 

Maswali 

  1. Ni sababu ipi inayomfanya popo akatae ya kuwa yeye si ndege? 
  2.  Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi huitwaje? 
  3. Katika ubeti wa pili popo anasema, “sina jadi na kunguru”, usemi “sina jadi” una maana gani?
  4. Kutokana na shairi hili, unadhani ni tuhuma gani zilikua zinamkabili popo?  v.
  5. “Hakimu makini, hadhira shauku tua”. Unaelewa nini kuhusiana na neno hadhira?

 

SEHEMU C : UTUNGAJI (ALAMA 10) 

Ichunguze barua rasmi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata;- 

Shule ya Msingi 

Ugele, 

S.L.P. 165, 

RINGO 

Tafadhali husika na barua hii. Mimi ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule yako. Ninaomba ruhusa ya kushiriki mashindano ya kanda ambayo yatafanyikia katika uwanja wa Samora siku ya Alhamis. Mashindano hayo yataanza mnamo saa 2:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 8:30 mchana. Ahsante 

6. Baada ya kukamilisha kuiandika barua hiyo Lashack aliambiwa na mwalimu wake kuwa barua yake ina mapungufu mengi na kuifanya ikose sifa za kuitwa barua rasmi. Taja vipengele vitano vinavyokosekana katika barua hii. 

i. 

ii. 

iii. 

iv.

 v. 

 

Maisha ni vita daima. Wewe ni bunduki. Akili, juhudi na maarifa ndizo risasi ambazo kila binadamu ametunukiwa na Mungu. Kila mmoja alipewa silaha hizo kwa kuwa aliyetuumba alitaka tukapambane vilivyo. Inaaminika hakuna cha bure katika dunia hii. Unataka mali? Unataka gari? Unataka nyumba nzuri? Basi pambana vilivyo. Mwanafunzi upo shuleni ili kunoa silaha zako vyema. Tumieni vyema muda wenu shuleni kwa kusoma ili msijejuta mtapokuja kutana na maisha. Hakuna chuo au shule utakayoenda kusomea maana ya maisha. Ila maisha utakutana nayo kadri unavyoishi. Ukizubaa maisha yatakufundisha maana ya maisha. Ukikubali kufundishwa maana ya Maisha na Maisha basi jua ya kuwa umekwisha. Huna jeuri tena! 

Maisha ni vita daima. Wewe ni bunduki. Akili, juhudi na maarifa ndizo risasi ambazo kila binadamu ametunukiwa na Mungu. Kila mmoja alipewa silaha hizo kwa kuwa aliyetuumba alitaka tukapambane vilivyo. Inaaminika hakuna cha bure katika dunia hii. Unataka mali? Unataka gari? Unataka nyumba nzuri? Basi pambana vilivyo. Mwanafunzi upo shuleni ili kunoa silaha zako vyema. Tumieni vyema muda wenu shuleni kwa kusoma ili msijejuta mtapokuja kutana na maisha. Hakuna chuo au shule utakayoenda kusomea maana ya maisha. Ila maisha utakutana nayo kadri unavyoishi. Ukizubaa maisha yatakufundisha maana ya maisha. Ukikubali kufundishwa maana ya Maisha na Maisha basi jua ya kuwa umekwisha. Huna jeuri tena! 

Maisha ni vita daima. Wewe ni bunduki. Akili, juhudi na maarifa ndizo risasi ambazo kila binadamu ametunukiwa na Mungu. Kila mmoja alipewa silaha hizo kwa kuwa aliyetuumba alitaka tukapambane vilivyo. Inaaminika hakuna cha bure katika dunia hii. Unataka mali? Unataka gari? Unataka nyumba nzuri? Basi pambana vilivyo. Mwanafunzi upo shuleni ili kunoa silaha zako vyema. Tumieni vyema muda wenu shuleni kwa kusoma ili msijejuta mtapokuja kutana na maisha. Hakuna chuo au shule utakayoenda kusomea maana ya maisha. Ila maisha utakutana nayo kadri unavyoishi. Ukizubaa maisha yatakufundisha maana ya Maisha. Ukikubali kufundishwa maana ya Maisha na Maisha basi jua ya kuwa umekwisha. Huna jeuri tena! 

Maisha ni vita daima. Wewe ni bunduki. Akili, juhudi na maarifa ndizo risasi ambazo kila binadamu ametunukiwa na Mungu. Kila mmoja alipewa silaha hizo kwa kuwa aliyetuumba alitaka tukapambane vilivyo. Inaaminika hakuna cha bure katika dunia hii. Unataka mali? Unataka gari? Unataka nyumba nzuri? Basi pambana vilivyo. Mwanafunzi upo shuleni ili kunoa silaha zako vyema. Tumieni vyema muda wenu shuleni kwa kusoma ili msijejuta mtapokuja kutana na maisha. Hakuna chuo au shule utakayoenda kusomea maana ya maisha. Ila maisha utakutana nayo kadri unavyoishi. Ukizubaa maisha yatakufundisha maana ya Maisha. Ukikubali kufundishwa maana ya Maisha na Maisha basi jua ya kuwa umekwisha. Huna jeuri tena! 

Maisha ni vita daima. Wewe ni bunduki. Akili, juhudi na maarifa ndizo risasi ambazo kila binadamu ametunukiwa na Mungu. Kila mmoja alipewa silaha hizo kwa kuwa aliyetuumba alitaka tukapambane vilivyo. Inaaminika hakuna cha bure katika dunia hii. Unataka mali? Unataka gari? Unataka nyumba nzuri? Basi pambana vilivyo. Mwanafunzi upo shuleni ili kunoa silaha zako vyema. Tumieni vyema muda wenu shuleni kwa kusoma ili msijejuta mtapokuja kutana na maisha. Hakuna chuo au shule utakayoenda kusomea maana ya maisha. Ila maisha utakutana nayo kadri unavyoishi. Ukizubaa maisha yatakufundisha maana ya Maisha. Ukikubali kufundishwa maana ya Maisha na Maisha basi jua ya kuwa umekwisha. Huna jeuri tena! 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 92

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MTIHANI WA KUJIPIMA KWA MSINGI

NUSU MUHULA WA PILI

KISWAHILI DARASA LA SABA.  AGOSTI, 2023

JINA LA MTAHINIWA_________________________________________________________________

 

SEHEMU: A – SARUFI

Chagua herufi ya jibu sahihi zaidi na uiandike kwenye kisanduku

  1. Juma alikuwa anacheza. Neno “alikuwa” ni aina gani ya kitenzi? _____ A. kikuu B. kisaidizi C. kishirikishi D. cha kawaida                                                                                                                                                                                [         ]
  2. Jana Mzee Maganga alinunua_____ sokoni. A. samaki nyingi B. samaki mingi C. visamaki mingi D. samaki wengi                                                                                                                                      [         ]
  3.    Kama wote wangejibidiisha ______________ mitihani yao vizuri. A. wangefaulu B. wangalifaulu C. wangalifuzu  D. wasingefuzu                                                                                                                                                                   [         ]
  4. Walioiba nguo za shule wamekamatwa . Sentensi hii ipo katika nafsi gani? _____ A. ya kwanza wingi B. ya tatu umoja C. ya pili wingi D. ya tatu wingi                                                                                                                            [         ]
  5. Ehee! Kumbe wewe ndiye mwizi wa mahindi yangu. Katika sentensi hii kihisishi ni _________ A. kumbe B. wewe  C. Ehee D. mwizi                                                                                                                                                                 [         ]
  6. Mzee Juma ameishi Morogoro _____ miaka kumi.A. toka B. kwa C. tangu D. kipindi                                          [         ]
  7. “Tunaimba”, kiambishi kinachoonesha wakati ni _____ A. – na – B. tu – C. –imba D. – a –                                [         ]
  8. Neno lenye maana sawa na nneno “shuku” ni _____ A. fahamu B. elewa C. jua D. dhani                                  [         ]
  9. Mtoto wa ng’ombe ni ndama, mtoto wa nzige ni _____ A. kinzige B. tunutu C. kifaranga D. njiwa                  [         ]
  10. Toni ameshindwa _____ wewe mfupi utaweza? A. lahaula B. angalau C. sembuse D. mbona                         [         ]
  11. Mzee Kufa amerejea jana. Neno “Kufa” limetumika kama _____ A. nomino B. kivumishi C. kitenzi D. kiunganishi                                                                                                                                         [         ]
  12. Tendo la kuamka asubuhi na mapema huitwa _____ A. wahi B. damka C. wasili D. jihami                               [         ]
  13. Umoja wa neno “nyaraka” ni _____ A. waraka B. miwalaka C. kiwaraka D. miwaraka                                       [         ]
  14. Mnyororo umekatika. Sentensi hii iko katika kauli gani? _____ A. kutendeka B. kutendwa C. kutendeana D. kutendewa                                                                                                                                                                          [         ]
  15. Neno lisilohusiana na mengine kati ya haya ni _____ A. maembe B. mapera C. maparachichi D. mchungwa                                                                                                                                          [         ]
  16. Mwanafunzi huyu ni mwaminifu. Neno “huyu” ni _____ A. kihisishi B. kielezi C. kivumishi D. kiwakilishi                                                                                                                                          [         ]
  17. Neno linaloingizwa kwenye kamusi ili lipatiwe maana huitwaje? _____ A. nomino B. kidahizo C. kitomeo D. kitenzi                                                                                                                                                                                   [         ]
  18. Madawati yetu yametengenezwa vizuri. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno? _____ A. kielezi B. kivumishi C. kitenzi D. kiunganishi                                                                                                                                  [         ]
  19. Kijana yule angalighani shairi, _____ mtukutu. A. angekuwa B. asingelikuwa C. asingekuwa D. asingalikuwa                                                                                                                                      [         ]
  20. Ubeti wa shairi wenye mistari minne huitwa _____ A. kibwagizo B. kituo C. mshororo D. tarbia                    [         ]
  21. Kobe hutembea “taratibu”. Neno taratibu limetumika kama _____ A. kivumishi B. kielezi C. kitenzi D. kiwakilishi                                                                                                                                     [         ]
  22. Wingi wa neno ulimi ni _____ A. maulimi B. ndimi C. ndimizi D. vidimi                                                                [         ]
  23. Mwanume mzee sana hujulikana kama _____ A. ajuza B. shaibu C. bibi  D.kijakazi                                           [         ]
  24. Nomino inayotokana na neno “zaa” ni _____ A. zaliwa B. zalisha C. mzawa D. mzazi                                        [         ]
  25. Mchezaji “maarufu” ameingia uwanjani. Neno maarufu limetumika kama _____ A. kisifa B. kielezi C. kivumishi D. kitenzi                                                                                                                                                         [       ]

 

 

 

 

SEHEMU: B – METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

Chagua herufi ya jibu sahihi zaidi na uindike kwenye kisanduku au jaza nafasi zilizoachwa wazi

  1. Bibi yake Juma ana umri wa miaka mia moja. Kwa umri huo _____ A. anakaribia kufa B. ni kibogoyo C. amekula chumvi nyingi D. hajui afanyalo                                                                                                                                       [         ]
  2. Ipi ni maana sahihi ya kitendawili “kulia kwake ni kicheko kwetu”? _____ A. maji B. mafuta C. machozi D. mvua                                                                                                                           [         ]
  3. “Upele humwota asiye na kucha”. Methali ipi kati ya hizi ina maana sawa na hiyo? _____ A. damu nzito kuliko maji B. penye miti hakuna wajenzi C. mwenda pole hajikwai D. dau la mnyonge haliendi joshi                                                                                                                                                   [         ]
  4. Eleza maana ya nahau “ana mkono wa birika”. _____ A. mchoyo B. wizi C. mpole D. mkono wa chuma                                                                                                                                       [         ]
  5. Uso wa samaki hausikii _____ A. maji B. viungo C. harufu D. vipodozi                                                                  [         ]
  6. Dira ya binadamu ni __________________________________________________________ ( malizia)

SEHEMU: C – USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo

Ni njaa kuondolewa, ukawa huna mshiko

Watuo ukafiwa, ukasalia na yako

Siku ukijatolewa, msiwe na mwenzi wako

Hapo utaona mwako, utakuliza ukiwa

Utakuliza ukiwa, likupatalo sumbuko

Wakati umelemewa, sipo kitandani mwako

Huna unayemjuwa, mbali na kwenu uliko

Hapo utaona mwako, utauliza ukiwa

Maswali 

  1. Shairi ulilosoma lina beti ngapi? ________________________________________________________________
  2. Vina vya kati na vya mwisho katika shairi hili ni ____________________________________________________
  3. Jina la mstari wa mwisho katika kila ubeti huitwa kituo, kitoshelezo au _________________________________
  4. Katika mstari wa kwanza wa kila ubeti una mizani ngapi? ___________________________________________
  5. Andika kitoshelezo (kituo) cha shairi hili. _________________________________________________________

SEHEMU: E – UTUNGAJI

Zipange sentensi zifuatazo zilete mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D

  1. Dakika chache baadaye tuliona msafara wa magari ukiingia.                                                                                  [         ]
  2. Mnamo saa saba hivi tuliona pikipiki ya askari wa usalama barabarani ikija mbio kama mshale.                    [         ]
  3. Mbele ya msafara huo kulikuwa na pikipiki nne zilizofuatana na gari la king’ora.                                               [         ]
  4. Ilikuwa ni siku ya alhamisi tulivu, tulikuwa tumeketi kibarazani.                                                                            [         ]

SEHEMU: E – UFAHAMU

Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata

Katika ndege wanaofugwa na binadamu jogoo ni mojawapo, ndege wengine ni kuku, bata, gegedu na njiwa. Lakini muungwana kuliko wote ni jogoo ambaye huwika usiku karibu na alfajiri kumwamsha binadamu ajizatiti na ratiba ya siku inayofuata. Lakini gegedu ni mzembe kuliko wote pia ni mchafu.

Maswali

  1. Ndege muungwana kuliko wote wafugwao ni _____________________________________________________
  2. Gegedu ni dume la ___________________________________________________________________________
  3. Neno “kujizatiti” kama lilivyotumika lina maana ya _________________________________________________
  4. Taja faida mojawapo ya ndege wafugwao na binadamu______________________________________________
  5. Kichwa kifaacho cha habari hii ni ________________________________________________________________

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 83

OFISI YA RAISI

WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI

MTIHANI WA  MUHULA WA KWANZA –MEI 2023

KISWAHILI – DARASA LA SABA

MUDA 1:30 MASAA

JINA ..................................................................  SHULE ...................................

MAELEZO

  1. Karatasi hii ina kurasa nne zenye maandishi yenye sehemu, A, B, C, D na E zenye maswali arobaini na tano (45)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
  3. Kumbuka kuandika majina yako, na shule yako kwenye karatasi ya kujibia
  4. Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
  5. Tumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi kwa maswali yote uliyopewa.

SEHEMU A

Sikiliza kwa makini habari inayosomwa na msimamizi kisha jibu maswali 1 – 5 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuandika katika karatasi ya kujibia.

 

Utalii ni aina ya biashara. Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea hutumia biashara hii kama chanzo cha mapato. Nchi hizi zina vivutio vya utalii kama vile wanyama pori, milima mirefu, fukwe za kuvutia, mito na maziwa. Watalii hutumia pesa kwa ajili ya chakula, malazi, usafiri na mambo mengine. Kwa njia hii, nchii inayotembelewa na watalii hujipatia pesa nyingi.

 

  1. ............. ni aina ya biashara


  1. Ufugaji
  2. Usafiri
  3. Utalii
  4. Biashara
  5. Wanyama pori


  1. Kipi kati ya vifuatavyo si katika vivutio vya utalii?
  1. Wanyama pori
  2. Milima mirefu
  3. Mito
  4. Maziwa
  5. Watalii
  1. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea hutumia utalii kama ............
  1. Chanzo cha mapato
  2. Biashara
  3. Chakula
  4. Mavazi
  5. Usafiri
  1. Nchi inayotembelewa na watalii hufaidika kwa .....
  1. Burudani
  2. Chakula
  3. Malazi
  4. Utalii
  5. Pesa nyingi
  1. Kwa nini baadhi ya nchi hutembelewa na walii?
  1. Kwa sababu ni kubwa
  2. Kwa sababu ni nchi zilizoendelea
  3. Kwa sababu ni nchi zinazoendelea
  4. Kwa sababu zina watu wengi
  5. Kwa sababu zina vivutio vya utalii

 

Chagua herufi ya jibu sahihi na kisha andika katika karatasi ya kujibia.

 

  1. Yule msichana anaimba vizuri. Neno lililopigwa mstari limetumika kama aina ipi ya maneno?
  1. Nomino
  2. Kielezi
  3. Kitenzi
  4. Kivumishi
  5. Kiwakilishi
  1. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ipo katika kauli halisi?
  1. Mimi siendi
  2. Alisema haendi
  3. Ameenda.
  4. Alisema hataenda
  5. Alisema anaenda
  1. Nomino inayotokana na kitenzi “vaa” ni ipi?
  1. Nguo
  2. Valisha
  3. Kivalo
  4. Kivazi
  5. Vazi
  1. Neno lipi linakamilisha sentensi isemayo. Timu ya Taifa ingalicheza vizuri ....... mchezo.
  1. Ingelishinda
  2. Ingeshinda
  3. Ingashinda
  4. Ingalishinda
  5. Itashinda
  1. Siku ya Mei Mosi wafanyakazi walipita mbele ya Waziri Mkuu wakishikilia ..... yenye maneno ya kuhimiza kazi. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?
  1. Mabango
  2. Libango
  3. Kibango
  4. Vibango
  5. Bango
  1. “Nguo yangu imechafuka sana.” Wingi wa sentensi hii ni upi?
  1. Nguo yangu imechafuka sana
  2. Nguo zetu zimechafuka sana
  3. Nguo yetu zimechafuka sana
  4. Nguo zao zimechafuka sana
  5. Nguo letu limechafuka sana
  1. Lipi kati ya maneno yafuatayo halina uhusiano na mengine?
  1. Ng’ombe
  2. Mbuzi
  3. Simba
  4. Chiriku
  5. Nyani
  1. Samaki, dagaa na nyama. Kwa neno moja huitwaje?
  1. Kitoweo
  2. Mboga
  3. Mchuzi
  4. Mlo
  5. Chakula
  1. Sentensi isemayo, “Itakapofika mchana .............. kuondoka” inakamilishwa kwa usahihi na neno lipi kati ya yafuatayo?
  1. Tuliruhusiwa
  2. Tutaruhusiwa
  3. Tumeruhusiwa
  4. Huruhusiwa
  5. Tunaruhusiwa
  1. Kinyume cha neno “duni” ni kipi?
  1. Thamani
  2. Kidogo
  3. Hafifu
  4. Kikubwa
  5. Imara
  1. Mzee Jumbe aliwapa wanae mawaidha juu ya maisha yao. Neno lililopigwa mstari lina maana gani?
  1. Mawazo
  2. Urithi
  3. Maonyo
  4. Mahubiri
  5. Hotuba
  1. Mtu anaesimamia kazi za shamba huitwaje?
  1. Nokoa
  2. Mnyapara
  3. Msimamizi
  4. Kiongozi
  5. Kiranja
  1. Pondamali ni kijana mwenye hila sana. Kisawe cha neno “hila” ni kipi?
  1. Hasira
  2. Ulafi
  3. Udanganyifu
  4. Ukorofi
  5. Ukabila
  1. “Jioni bahari ilikuwa ......... kwa hiyo wavuvi walivua samaki bila wasiwasi. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?
  1. Kupwa
  2. Shwari
  3. Kavu
  4. Baridi
  5. Joto
  1. Mama alijifunza kuendesha gari lakini bado hajafuzu. Neno “hajafuzu” lina maana ipi kati ya zifuatazo?
  1. Hajajua kuendesha
  2. Hajamaliza mafunzo hayo
  3. Hajapata leseni
  4. Hajahitimu mafunzo hayo
  5. Hatamaliza mafunzo haya
  1. “Kidole kimoja hakivunji chawa”. Methali hii ina maana sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?
  1. Mchagua jembe si mkulima
  2. Kilema si ugonjwa
  3. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  4. Kuvunja kwa pakacha nafuu kwa mchukizi
  5. Kulia kwake ni kicheko kwetu
  1. Kifungu kipi cha maneno hukamilisha kitendawili kifuatacho kwa usahihi? Watoto wa binadamu ...................
  1. Huondoka na kurudi
  2. Wakiondoka hawarudi
  3. Hutangulia kuondoka
  4. Huchelewa kuondoka
  5. Huondoka pamoja na binamu.
  1. “Sina hali”. Nahau hii ina maana gani?
  1. Sina pesa
  2. Ninaumwa
  3. Sina ahueni
  4. Sijambo
  5. Sijiwezi
  1. “Udongo uwahi ungali maji” Methali hii ina maana gani?
  1. Udongo ukikauka unakuwa mgumu
  2. Kuchukua tahadhari kabla ya hatari
  3. Usitatue tatizo kabla ya hatari
  4. Udongo wenye maji usiuwahi
  5. Kukimbilia tatizo si kulitatia
  1. Tatizo la ufisadi limeota mizizi katika nchi yetu. “Kuota mizizi” ni usemi wenye maana gani?
  1. Kuibuka
  2. Kutoweka
  3. Kufifia
  4. Kuanza
  5. kushamiri
  1. “Mgonjwa aendapo hospitalini hapewi matibabu hadi ato chochote kwa mhudumu wa afya.” Nahau ipi inaelezea hali hiyo?
  1. Kutia mkono kizani
  2. Kuzunguka mbuyu
  3. Kuua tembo kwa ubua
  4. Kujikaza kisabuni
  5. Kutoa ni moyo
  1. Katika methali zifuatazo ni methali ipi ambayo haifanani na zingine?
  1. Mlilala handingwandingwa mwenye macho haambiwi tule
  2. Usimwamshe aliyelala
  3. Mwenye uchungu hambiwi liwa.
  4. Asiyeuliza hanalo ajifunzalo
  5. Mtaka cha mvunguni sharti ainame
  1. Neno lipi linakamilisha methali isemayo: Ndugu chungu jirani? ......
  1. Ndugu
  2. Rafiki
  3. Jamaa
  4. Mkungu
  5. Kinu
  1. Tegu kitendawili kisemacho “Ajihami bila silaha”kwa kuchagua neno sahihi kati ya yafuatayo:
  1. Nyoka
  2. Mbwa
  3. Kinyonga
  4. Paka
  5. Mjusi
  1. Tegua kitendawili kisemacho “Maskini huyu hata umchangie namna gani haridhiki”, kwa kuchagua neno moja kati ya yafuatayo:
  1. Tumbo
  2. Macho
  3. Pua
  4. Masikio
  5. Mdomo

 

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 31 – 35 kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.

 

  1. Heshima kitu muhimu, anachohitaji mtu

Inatakiwa kwa hamu, ili kuujenga utu,

Jambo hili ufahamu, usijedharau mtu

Ukitaka heshimiwa, nawe heshimu wengine

 

  1. Huinunui heshima, bure inapatikana

Wewe uyatende mema, fanaka kwake Rabana 

Mdogo hata mzima, onyesha pendo mwanana

Ukitaka heshimiwa, nawe heshimu wengine.

 

  1. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi?
  1. Nne
  2. Tatu
  3. Moja
  4. Mbili
  5. Sita
  1. Mshororo mmoja wa ubeti una jumla ya mizani ngapi
  1. 8
  2. 6
  3. 16
  4. 10
  5. 12
  1. Neno Rabana katika ubeti wa pili linamtaja nani?
  1. Mungu
  2. Miungu
  3. Mfalme
  4. Baba
  5. Malenga
  1. Kibwagizo au kiitikio cha shairi hili ni;
  1. Uheshimu watu
  2. Heshima kitu cha bure
  3. Ukitaka heshimu wengine
  4. Heshima
  5. Ukitaka heshima nawe heshimu wengine.
  1. Kichwa cha shairi hili ni:
  1. Kupata heshima
  2. Heshima
  3. Heshimu wengine
  4. Dira ya heshima
  5. Heshima ni utu

 

SEHEMU B

UTUNGAJI

Umepewa Insha yenye sentensi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili kujibu maswali 36 – 40 

 

  1. Tutaendela kusaidiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali hasa katika shughuli za kiuchumi, kielimu na kijamii
  2. Kumekuwa na mwingiliano wa tamaduni za kigeni katika nchi zetu mfano mavazi, lugha, ngoma, nyimbo, mila, na desturi.
  3. Lakini katika kijiji chetu cha tupendane tumeamua kudumisha upendo na ushirikiano miongoni mwetu
  4. Baadhi ya misingi mizuri ya maisha imevurugwa
  5. Mambo mengi yaliyotokea na yanayoendelea kutokea yameathiri sehemu ya utamaduni wetu.

 

SEHEMU C

UFAHAMU

Soma habari ifuatayo halafu jibu maswali (41 – 45) kwa kuandika jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

 

Kijana Makubwa alikuja juu katika kushikilia tabia yake ya ufedhuli na maringo. Kwa kuwa alikuwa msomi, hakudiriki kufumbata jembe na kulima shambani pamoja na wazazi wake. Yeye katika mawazo yake aliona kuwa alihusika na kwenda mjini kutafuta ya ukarani. Aidha Makubwa alikuwa akiwaudhi wengi kijijini, alipozungumza nao aliwamung’unyia Kiswahili kwa majivuno na ukaidi sana. Matendo na mwendo wake vilionesha kuwa alijiona mtu wa maana sana kuliko wengine na alijawa na mawazo kemkem ya ukubwa wa Madaraka.

 

Shuleni kwake, kama kijijini, Makubwa alipeanda maisha ya huria, kutenda lolote alilotaka akilini mwake. Mara nyingi alikuwa kiguu na njia, hakupenda kutulia mahali pamoja. Alikuwa hajali sheria,aliamka, alisomea alipopataka na kujivali alivyotaka. Yeye kila wakati alipenda starehe. Kazi alikuwa hafanyi, hata akazoea kusingizia mvua kwa kila wajibu ambao hakuutimiza. Lakini siku zake arobaini ziliwadia, shule haikuweza kumvumilia tena kijana Makubwa aliyependa huria kuliko nidhamu iliyokubalika na wengi. Shuleni kwake alipigwa kalamu nyekundu. Bila shaka kijijini walianza kusema, “Aliye juu mgoje chini”. Wengine walisema “Msiba wa kujitakia hauna kilio”

 

MASWALI

  1. Makubwa hakuweza shughuli za kilimo kwa sababu .............
  2. Makubwa alikuwa na tabia gani ambayo haikupendeza huko shuleni? .........
  3. Mwandishi anasema, “Alijawa na mawazzo kemkem ya ukubwa wa Madaraka” Maana ya neno kemkem ni ipi? .......................
  4. Kwa maoni yako kichwa habari hii kinaweza kuwa kipi? ...........
  5. Fundisho unalolipata katika habari hii ni “Wanafunzi tuwe na: ...............

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 73

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA SEPT 2022

KISWAHILI  DARASA LA SABA. 

 

SEHEMU A: SARUFI

CHAGUA JIBU SAHIHI

  1. Nimeishi hapa Mwanza..........................ishirini na tano 
    A.tangu miaka B. kuanzia miaka C.kwa miaka D.nina miaka E.hata miaka
  2. .Neno “mchakamchaka” lina aina ngapi za irabu?

     A. nne B.sita C.mbili D.kumi na mbili E.moja

  1. Sentensi “paka atamla panya”ipo katika wa kati gani? A.uliopo B.usiodhihirika C.ujao D.mtimilifu E.uliopita
  2. Mchague.........................umpendaye 
    A.yoyote B.wowote C.yeyote D.wote E.vyovyote
  3. Ikiwa utakuja kesho........................

     A.ukinikuta B.ungenikuta C.utamkuta D.utakapomkuta E.umenikuta

  1. .Sikupenda.......................ndiomaanasikumjibu

      A.maudhi B.udhia C.mauzi D.tatizo E.kuuzika

  1. Mahakama ili bidi.............matokeo ya uchaguzi baada ya mlalamikaji kushinda kesi 
    A.ibainishe B.ibatilishe C.ibadilishe D.iahilishe E.isainishe
  2. Ng’ombe dume aliyehasiwa ambaye hutumika kulima huitwa.................

     A.fahari B.maksai C.beberu D.fahali E.mbuguma

  1. Lipi kati ya maneno yafuatayo halilandani na mengine? A.mpera B.papai C.limao D.chungwa E.pera
  2. Hali yakutokuwa na mali yoyote huitwa.......................
    A.ukwasi B.ufukara C.ubahili D.ukuta E.utajiri
  3. Ukitaka kufanya vizuri katika mitihani yako....................kusoma kwabidii 
    A.hunabudi B.unabudi C.nibudi D.siobudi E.budi
  4. Chama chetu ndicho kinachoshika hatamu sentensi hii iko katika ngeli ya ..............

     A. a-wa B.ki-vi C.li-ya D.i-zi E.u-ya

  1. Katika neno “mkulima”mzizi wa neno ni.................

       A.-kul- B.-li- C.lima D.-lim- E.-uli-

  1. “Amina ni mvivu sana“ katika sentensi hii neno “ni” limetumika kama aina ipi ya maneno? A.kiunganishi B.kivumishi C.kitenzi D.nomino E.kiwakilishi
  2. ”Osheni vyombo haraka “hii ni kauli gani?

     A.taarifa B.kutenda C.halisi D.amri E.tata

  1. Hadi sasa hakuna mwanafunzi________________aliyeingia kidato cha kwanza.

    A. yoyote B. wowote C. yeyote D. yote E. yeote

  1. .Kujishughulishashughulisha ni neno lenye aina ngapi za irabu? 
     A.Kumi B. tatu C.Kumi na moja D. Kumi na tatu E.Tisa
  2. Neno lipi ni tofauti na mengine kati ya haya?

A.Katu B.kamwe C.asilani D.hidaya E.abadani

  1. Neno lipi kati ya haya lipo katika ngeli ya A-WA?

A.Jongoo B. mti C. yai D.simu E.Ugonjwa

  1. Kisawe cha kinyonga ni Lumbwi ,kisawe cha karainibeseni , kisawe cha mamba ni kipi 
     A.Nyangunya B. mando C.kiboko D. samaki E.ngwena

SEHEMU B: LUGHA VA KIFASIHI

CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

  1.              ”Mambo mema na mabaya hayafungamani” kifungu hiki cha maneno kinatoa maana ya methali ipi kati ya zifuatazo?

A.liwapo lako nijema ,la mwenzio ni baya B.lila na fila havita ngamani C.gongo la mbuyu simvule D. lako ni lako likikufika la mwenzako E.padogo pako si pakubwa pa mwenzako

  1.              Kamilisha methali ifuatayo “mwacha asili” ni.......................

A.mtalii B.mzalendo C.mkunga D.mtumwa E.mdaku

  1.              Mtu asemapo “ashakum si matusi” ana maana...........

 A.niwiye radhi kwa haya B.yafuatayo si matusi C.nakutukana usikasilike

D.hatutumii matusi kuongea E. asantekwamatusi

  1.              ”Ukitaka kuruka agana na nyonga” methali hii inatuasa nini?

A.uliza kabla ya kutenda B.tafakarikwa kina kabla ya kutenda C.tekeleza jambo kwa maelekezo D.fuatilia ndipo utende E.tenda jambo kwa kufuata maamuzi

  1.              Aliyekupigia simu katutoka.nini maana ya “katutoka”

A.kasafiri B. amekuja C. kaondoka D.katoroka E. kafariki

  1.              Nahau “motto wakikopo” inamaana gani?

 A. mbeba makopo B.mlevi C. muhuni D.mwizi E.anapendamakopo

  1.              Mfuauji ni mtu....................

A.mwongo B. mnene C. mkali D.mnywauji E. maridadi

  1.              Kuwanaulimiwaupangamaanayakeni.............

A.kutoa maneno makali B.usema uongo C.kupayuka D.kusema hovyo E.kuropoka

  1.              Kitendawilikipikatiyavifuatavyojibu lake sikinyonga ?

A.huu wanauzazi wake B.tajiri wa rangi C.napigwa faini kosa silijui

D.ajihami bila silaha E. huringahataakiwahatarini

  1.              Tegua kitendawili “mkutanapo ni marafiki muachanapo ni maadui”

A.kinyesi B.jambazi C. rafiki D.mume/mke E.kibaka

 

SEHEMU C: USHAIRI /UFAHAMU

SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA JIBU MASWALI

Leo ninawasilisha,haya unayosikia,

Wazazi wametuchosha haki zetu mwafukia, Ni kweli wametuchosha.tumekwishashitakia , Twaomba mtukidhie,haki hizi zaWatoto.

Asubuhi twaondoka ,shuleni kujisomea, Na shuleni tukifika,usafi ni mazoea,

Vinywa vyetu vinanuka, njaa kwetumazoea, Twaomba mtukidhie,haki hizi za Watoto.

Maswali 

  1.                   Shairi ulilosoma lina jumla ya beti..............

A.nne B.tatu C.tano D.nane E. mbili

  1.  Jumla ya mishororo katika beti zote za shairi ni............

A.8 B.16 C.10 D.12 E.4

  1.  Shairi hili ni ina ya.................

A.tathlitha B.takhmisa C.tarbia D.malumbano E.mapokeo

  1.                   Shairi hili linakituo 
    A.bahari B. sibahari wala nusu bahari C.nusubahari D. mkarara E.mkato
  2.                   Mstari wa mwisho katika kila ubeti hujulikana kama.....................

A.vina B.mizani C.kituo D.mshororo E.kituomkato

SEHEMU D: UTUNGAJI 

PANGA SIMU IFUATAYO KWA USAHIHI KWA KUTUMIA HERUFI A, B, C, D, E. 

  1.                   KALUMANZIRA
  2.                   PAMBE JALALA
  3.                   TEMEKE
  4.                   NIMEPATA UJUMBE WAKO
  5.                   S.L.P. 82

SEHEMU E: UFAHAMU. 

Soma habari ifuatayo na ujibu maswali ya nayofuata kwa umakiniIlikua ya pata saa kumi za jioni halaiki iliyokusanyika kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius

Kambarage Nyerere ilipolipuka kwa furaha baada ya ndege kubwa aina ya Dreamliner Boeing787 kutua uwanjani hapo. Wakiongozwa na kiongozi mkuu wa nchi, viongozi mbalimbali walisimama nakumuunga mkono Raisi kuilaki ndege hiyo.Tofauti nadhifa nyingine za kitaifa mara hii hata wananchi mikoani walisitisha shughuli zao nakuwasha runinga zao kushuhudia tukio hili la kipekee. Kwenye magari watu waliwasha rununu zao nakufuatilia kwa ukaribu zaidi huku wengine wakipoza makoo yao kwa sharubati baridi Hatimaye Raisi alisimama kwenye mimbari iliyoandaliwa nakutoa hotuba fupi muhimu akisisitiza watu kulipa kodi ili taifa letu liachane na utegemezi kiuchumi.

MASWALI

  1.                   Halaiki ya kuipokea ndege ilikusanyika wapi..................................
  2.                   Ni aina ipi ya ndege ilipokelewa siku hiyo?.................................
  3. Neno lipi limetumika badala ya mkusanyiko wa watu wengi au sherehe maalumu ambapo hotuba hutolewa nahuambatana na vyakula ?              
  4.                   Nini maana ya neno “rununu” kama neon hili lilivyotumika kwenye habari hii?......................
  5.                   kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari uliyoisoma ?.....................................

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 64

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA MWIGO DARASA LA SABA

KISWAHILI

MUDA:1:30                                                             

JINA_____________________________________SHULE_________________________

MAELEKEZO:

  1. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
  2. Kumbuka kuandika majina yako.
  3. Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.

SEHEMU A: FASIHI NA MSAMIATI

1   Hali ya kuwa na mali nyingi au fedha huitwa  

  1.    Ubahili b. ukwasi c. ukapa d. ukata e. ukachero
  1.    Mtoto mpole hupendwa na wanafunzi wenzake darasani. Neno ‘mpole’ limetumika kama
    1.    Kiwakilishi b. nomino c. kivumishi d. kielezi e. kiungo
  2.    “Ili tuendelee          kufanya kazi kwa bidii”. Neno lipi limekosekana ili kukamilisha sentensi
    1.    Ni budi b. hatuna budi c. tuna budi d. kuna budi e. hapana budi
  3.    “Maandishi yanasomeka vizuri”. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
    1.    Ujao b. uliopita c. mazoea d. uliopo e. timilifu
  4.    Hamza alikuwa anaimba tangu ujana wake. Neno ‘alikuwa’ ni aina gani ya kitenzi?
    1.    Kisaidizi b. jina c. kishirikishi d. kitegemezi e. sana
  5.    Mahindi, maharage, ufuta, michungwa, migomba na mihogo kwa neno moja huitwa
    1.    Mimea b. vyakula c. matunda d. mboga e. miche
  6.    Wale wanakimbia polepole. Neno ‘wale’ limetumika kama aina ipi ya maneno?
    1.    Nomino b. nafsi c. kiwakilishi d. kielezi e. kitenzi
  7.    Neno lipi kati ya maneno yafuatayo ni kinyume cha neno ‘hobelahobela’?
    1.    Faragha b. ovyo ovyo c. vizuri d. mpangilio e. ubaya
  8.    Neno moja linalojumuisha herufi a, e, i, o na u ni lipi?
    1.    Silabi b. konsonanti c. mwambatano d. irabu e. kiambishi
  9. Mzizi wa neno “amenichora” ni          
    1.    –achor- b. –nichor- c. –chorea- d. –amenich- e. –chor-
  10. Mabomba ya kupitisha moshi toka jikoni kwenda nje huitwa
    1.    Bahari b. dohari c. ghala d. hosteli e. boya
  11. Wingi wa sentensi “Yule mwali hali wali” ni      
    1.    Wale wali hali wali
    2.    Wale wali hawakuli wali
    3.     Wale wanawali hawali wali
    4.    Wale wali hawali wali
    5.    Wale wali hajala
  12. Kama angelilima shamba kubwa           
    1.    Angevuna mazao mengi
    2.    Angelivuna mazao mengi
    3.     Angalelivuna mazao mengi
    4.    Angalivuna mazao mengi
    5.    Atavuna mazao mengi
  13. Kalamu zako ni nzuri. Ukienda dukani uninunulie         . Kifungu kipi cha maneno hukamilisha sentensi hiyo?
    1.    Kama hivyo
    2.    Kama hicho
    3.     Kama hizo
    4.    Kama hiko
    5.    Mfano wa hicho
  14. Ni sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ipo katika kauli taarifa?
    1.    Tafadhali nichunie ng’ombe wangu
    2.    Nichunie ng’ombe wangu
    3.     Aliniomba nikamchunie ng’ombe wake
    4.    Nichunie ng’ombe tafadhali
    5.    Kwanini unanichunia ng’ombe wangu
  15. Neno ‘kuku’ liko katika ngeli ya aina gani?
    1.    KI – VI
    2.    A – WA
    3.     YU-A-WA
    4.    I-ZI
    5.    LI-YA
  16. “Ukitaka kuja unijulishe mapema”. Usemi huu ni aina gani ya sentensi?
    1.    Ambatano b. shurutia c. sahihi d. changamano e. sentensi fupi
  17. Penina huimba kila siku. Hii ni hali gani ya kitenzi?
    1.    Timilifu b. isiyodhihirika c. mazoea d. kuendelea e. kupita
  18. Kipi ni kisawe cha neno ‘tembo’?
    1.    Faru  b. ndovu c. nyati d. twiga e. mbogo
  19. Tulicheza ngoma na kuimba usiku kucha. Katika sentensi hii watenda ni nafsi ipi?
    1.    Ya tatu wingi b. ya pili wingi c. ya kwanza wingi d. ya pili Umoja  e. ya tatu Umoja SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI

Andika herufi ya jibu sahihi

  1. Siku hizi siri za mafisadi zimeanikwa juani. Usemi ‘kuanikwa juani’ una maana ipi kati ya hizi zifuatazo?
    1.    Kuelezwa waziwazi
    2.    Kusemwa hadharani
    3.     Kusemwa jukwaani
    4.    Kusemwa nje ya kikao
    5.    Kuelezwa hadharani
  2. “Kidagaa kimemuozea”. Msemo huu una maana gani?
    1.    Kukwepa kulipa deni


  1.    Kutowajibika kulipa
  2.     Kuelemewa na jambo
  3.    Kupoteza Tumaini
  4.    Kulipa deni maradufu
  1. Tegua kitendawili kisemacho “bibi kafa kaniachia pete”.
    1.    Konokono b. jongoo c. tandu d. nyoka e. mende
  2. Methali isemayo “Mgaagaa na upwa hali wali mkavu” inatoa funzo gani?
    1.    Bidii huleta mafanikio
    2.    Mafanikio ni matokeo ya kazi
    3.     Bidii huleta faraja
    4.    Bidii ni kazi ya kuhangaika
    5.    Mafanikio ni ya lazima
  3. Nazi yangu yafurahisha ulimwengu pia. Jibu la kitendawili hiki ni
    1.    Moto b. mwezi c. nyota d. jua e. mbingu
  4. Kuwa na ulimi wa upanga maana yake ni
    1.    Kutoa maneno makali
    2.    Kupayuka
    3.     Kutoa maneno ovyo
    4.    Kukata maneno
    5.    Kukataa katakata
  5. Maisha ya Abunuasi yalivyo ni sawa na kukalia kuti kavu. Maana ya kukalia kuti kavu ni ipi?
    1.    Kuwa mzee sana b. kuwa na maisha ya kimwinyi c. kuwa na maisha ya kipwani

d. kuwa na maisha ya kutegemea urithi e. maisha ya kutojishughulisha

  1. Mama ameandaa meza. Maana ya Nahau kuandaa meza ni
    1.    Kusafisha na kupamba meza b. kununua meza c. kuandaa chakula mezani

d. kusafisha meza e. kupamba maua meza

  1. Wana wa mfalme ni wepesi kujificha. Maana ya kitendawili hiki ni
    1.    Masikio b. macho c. pua d. ulimi e. ini
  2. Haraka haraka haina Baraka. Kinyume cha Methali hii ni
    1.    Polepole ndio mwendo
    2.    Mpanda ovyo hula ovyo
    3.     Mtoto umeleavyo ndivyo akuavyo
    4.    Asiyekuwepo na lake halipo
    5.    Ahadi ni deni

SEHEMU C: UTUNGAJI

Zipange sentensi zifuatazo zilizochanganywa ili zilete mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A, B, C na D

  1. Dakika chache baadaye tuliona msafara wa magari ukiingia
  2. Gari hilo lilifuatwa na gari lingine lillilojaa askari wa kuzuia fujo kisha lilifuata gari la Rais


  1. Mnano saa saba hivi tuliona pikipiki ya askari wa usalama barabarani ikija mbio kama mshale
  2. Mbele ya msafara huo kulikuwa na pikipiki nne zilizofuatwa na gari la polisi lenye

king’ora

 

SEHEMU D: UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu swali la 31 – 40 kwa kuandika herufi ya jibu sahihi

Umma ulipozinduka na wakawauliza wafalme walivyotajirika kinyume na matarajio ya umma, kulikuwa na vita……”watu wetu wanatuonea”. Watu hawakuwaelewa….hawakurudi nyuma, walichukua kilicho chao. Hii ndio hadithi ya kisiwa cha wafalme! Kijiji hicho kilikuwa na viwanda mbalimbali vilivyosaidia kujenga na kuinua uchumi wake.

Waliteuliwa wakurugenzi wa aina aina waliosaidiwa na watumishi wengi kukamilisha sera yao ya kazi lakini shetani mbaya – pesa! Alikuwa sehemu hii. Wakurugenzi walikula, wahasibu walikula, watumishi pia walikla. Kwa ufupi kila mtu alikula. Walipoona wanataka kushikwa kwa makosa ya kula kilicho cha umma, wakachoma moto kiwanda chao ili kupoteza ushahidi. Hasara ilibaki kwa umma. Wao wakaanzisha miradi iliyowalisha kwa kutumia pesa za umma.

Wengine nao walipoona hayo nao wakaiga. Matokeo yake vikajengwa vijiji kama vile vya wafalme. Umma pia ukashtuka, ukawauliza na kisha kuchukua haki zao kwa nguvu. Hivyo hadithi iliyotamba mwanzo ikawarudia tena watu hawa na ukweli ukabaki kuwa jamii isiyojua kiini cha matatizo yake haiwezi kuyatatua.

MASWALI

  1. Neno ‘kuzinduka’ kama lilivyotumika katika habari hii lina maana ipi?
  2. Umma ulivyoshtuka kwa mara ya pili uliamua             
  3. Shetani mbaya aliyetajwa katika habari hii ni              
  4. Shetani mbaya alikumba sehemu hii pia. Neno ‘shetani’ limetumika kama nomino ya aina

gani

  1. Katika habari hii hapa juu, Methali ipi inaweza kuwa na mafunzo sawa na habari hii hapo juu?
  2. Kisawe cha neno ‘utajiri’ ni                 

SEHEMU E: USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 41 hadi 46 kwa kuandika herufi ya jibu sahihi

Nami nashika kalamu, maana menilazimu. Nawataka mfahamu, kuhusu mambo muhimu, Maana mekuwa ngumu, kuachwa na wahujumu, Rushwa ni adui wa haki, wananchi tupingeni.

 

Mepewa majina mengi, lukuki yaso idadi, Maana walafi ni wengi, kila siku wanazidi, Waheshimiwa na wengi, wamekuwa wakaidi, Rushwa ni adui wa haki, wananchi tupingeni.

 

Inaitwa takrima, au chai ya mgeni, Mnapotaka huduma, basi mikono nyosheni, Na mkijiweka nyuma, huduma isahauni, Rushwa ni adui wa haki, wananchi tupingeni.

 

MASWALI

  1. Kichwa cha shairi hili chafaa kuwa

 

  1. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi?
  2. Neno ‘takrima’ kama lilivyotumiwa na mshairi lina maana gani?
  3. Vina vya kati vya shairi hili ni
  4. Kila ubeti wa shairi hili una jumla ya mizani

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 52


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINI DARASA LA VII JULAI 2021

KISWAHILI

Muda: saa 1 : 30

MAELEKEZO:

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

SEHEMU A: 

SIKILIZA KWA MAKINI HADITHI UTAKAY-OSOMEWA NA MSIMAMIZI.KISHA JIBU SWALI LA 1 – 5 

HADITHI

Hapo zamani za kale palikuwa na kijiji kiitwacho Faru. Faru ni kijiji kilichokuwa karibu na msitu mkubwa wenye wanyama wakali. Wanakijiji wa Faru waliishi maisha ya raha sana. Kiongozi wao aliitwa Adabu, alikuwa kiongozi shupavu na mzalendo. Wanakijiji walimpenda kwa sababu alikuwa anajitoa kwa ajili ya kijiji chake, alipenda haki na alipigania maendeleo ya kijiji chake. 

Siku moja Adabu akiwa nyumbani kwake alisikia kelele nje ya nyumba yake. Alipotoka nje aliona kundi kubwa la wanakijiji wameshikilia silaha mbalimbali kama vile rungu, sime na magongo, hakujua ni ya kazi gani? Akauliza kwa shauku “kuna nini?” Mzee Funzi akajibu kwa hofu “tumevamiwa! tumevamiwa! na simba. “Simba?” Adabu aliuliza huku akikimbia kurudi ndani, akatoka na mshale. Punde si punde ilisikika ngurumo nyuma ya nyumba yake. 

Adabu akawaambia “Msiogope” kisha akawagawa katika makundi mawili ili kumzunguka na kumshambulia simba. Baada ya kukuru kakara za muda mrefu wanakijiji walifanikiwa kumuua simba. “Ama kweli jifya moja haliinjiki chungu,” alisikika akisema kijana mmoja. Wanakijiji waliondoka kwa furaha na kila mmoja alirudi nyumbani. Mpaka sasa wanakijiji wa Faru wanaishi kwa amani na ushirikiano.

1. Adabu alikuwa Kiongozi mwenye tabia gani kati ya zifuatazo? ________ 

  1. Mwongo na shupavu 
  2. Shupavu na mwoga 
  3. Mkakamavu na mvivu 
  4. Shupavu na mzalendo 
  5. Mpenda raha sana     [       ]

2. Kwa nini Adabu alipendwa na Wanakijiji? ______________ 

  1. Alipenda haki 
  2. Aliua simba 
  3. Alikuwa na mshale 
  4. Alikuwa na nguvu 
  5. Alikuwa msomi     [       ]

3. Nani alipiga kelele akisema tumevamiwa na simba? ____ 

  1. Wanakijiji 
  2. Mzee Funzi 
  3. Kijana
  4. Adabu 
  5. Kiongozi

4. Kwa nini Adabu aliwagawa wanakijiji katika makundi mawili? _______ 

  1. Wamfukuze simba 
  2. Wamuue simba 
  3. Wamuone simba 
  4. Wamtege simba 
  5. Wamtishie simba

5. Je unapata funzo gani kutokana na hadithi uliyoisikiliza? ________ 

  1. Tunapaswa kushirikiana 
  2. Ni lazima kumpiga simba 
  3. Ni vizuri watu kukusanyika 
  4. Tunapaswa kubeba silaha 
  5. Ni lazima kumuua simba     [       ]

6. Mtu asiyepokea ushauri wa wengine huishia kuharibikiwa katika maisha. Ni methali ipi kati ya zifuatazo itafaa kufikisha ujumbe huu? _______ 

  1. Asiyekuwepo machoni na moyoni hayupo. 
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
  3. Asiye na mengi ana machache. 
  4. Asiyeangalia huishia ningalijua. 
  5. Asiyeuliza hana ajifunzalo     [       ]

7. “Mama alimwagiza Chitemo, “Nenda ukanunue mboga za majani.” Sentensi hii ipo katika kauli ipi kati ya zifuatazo? __ 

  1. Taarifa 
  2. Mazoea 
  3. Halisi
  4. Tata
  5. Mbiu     [       ]

8. Katika maneno yafuatayo neno lipi halilandanina mengine? ________________________ 

  1. Ndovu 
  2. Mbogo 
  3. Faru 
  4. Korongo 
  5. Nyumbu     [       ]

9. “Akibeba watoto hawezi kuwashusha.” Maana ya kitendawili hiki ni sawa na kitendawili kipi kati ya hivi? _____ 

  1. Hausimami hausimiki 
  2. Mjomba hataki tuonane 
  3. Pazia la Mungu 
  4. Bomu la machozi 
  5. Babu amelala ndani ndevu ziko nje.     [       ]

10. Tumemsikia Nadi akisema, “Mimi huwa ninapenda kusoma jioni.” Sentensi ipi kati ya zifuatazo inatoa taarifa ya alichokisema Nadi? ____ 

  1. Nadi alisema kuwa yeye huwa anapenda kusoma jioni. 
  2. Nadi alisema kuwa mimi huwa napenda kusoma jioni. 
  3. Nadi alisema kuwa yeye alikuwa anapenda kusoma jioni. 
  4. Nadi alisema kuwa mimi nilikuwa ninapenda kusoma jioni 
  5. Nadi alisema kuwa weweunapenda kusoma jioni.     [       ]

11. Migodela alipopata taarifa ya msiba,alirudi nyumbani na kukuta msiba umekwisha. Ni nahau gani inaweza kutumika kueleza hali hiyo kati ya hizi? ______________ 

  1. Kaa kitako 
  2. Anua matanga 
  3. Enda jongomeo 
  4. Kusanya virago 
  5. Kata shauri.     [       ]

12. Katika sentensi “Shangazi alimwambia kuwa atakapopata nauli atakuja kijijini”, mzungumzaji ametumia nafsi gani kati ya hizi? ________________________ 

  1. Nafsi ya pili wingi
  2. Nafsi ya tatu wingi 
  3. Nafsi ya tatu umoja 
  4. Nafsi ya pili umoja 
  5. Nafsi ya kwanza wingi     [       ]

13. Selule ni kijana mchapakazi hodari aliyelima bustani kubwa ya mboga za majani kisha kuuza na kujipatia fedha za kutosha. Ni methali ipi kati ya hizi inafaa kuelezea hali hii? _____________________ 

  1. Simba mwenda pole ndiye mla nyama. 
  2. Mchumia juani hulia kivulini
  3. Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
  4. Mpanda hovyo hula hovyo. 
  5. Mla mla leo mla jana kala nini?     [       ]

14. Babu alisema “Kilimo ni uti wa mgongowa taifa letu.” Je babu alimaanisha nini kati ya yafuatayo? _____________ 

  1. Kilimo hakitegemewi 
  2. Kilimo kinategemewa 
  3. Kilimo hakifurahishi 
  4. Kilimo kinafurahisha 
  5. Kilimo kinachosha

15. “Afadhali jirani mchawi _________.” Ni kifungu kipi kati ya vifuatavyo kinakamilisha methali hii kwa usahihi? 

  1. kuliko mlevi 
  2. kuliko mjeuri 
  3. kuliko mmbea 
  4. kuliko mwongo 
  5. kuliko mnafiki     [       ]

16. “Nyafu alipotoka kazini alianza kukata maji hadi usiku wa manane.” Je Nyafu alifanya nini kati ya mambo yafuatayo? __ 

  1. Alikunywa uji 
  2. Alikunywa chai 
  3. Alikunywa pombe
  4. Alikunywa maziwa
  5. Alikunywa maji     [       ]

17. Pembua ana tabia ya kumwaga chakula kinachobaki baada ya kushiba. Je utatumia methali ipi kati ya zifuatazo kumshauri Pembua aache tabia hiyo? _______________ 

  1. Nyongeza haigombi. 
  2. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. 
  3. Akiba haiozi. 
  4. Haba na haba hujaza kibaba.
  5. Usiache mbachao kwa msala upitao     [       ]

18. Baba yangu ni “MHADHIRI” wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Je, Baba yangu anafanya kazi gani kati ya hizi zifuatazo? _____ 

  1. Anasoma masomo ya Chuo Kikuu 
  2. Anasajili wanafunzi wa Chuo Kikuu 
  3. Anafundisha wanachuo wa Chuo Kikuu 
  4. Anafuatilia nidhamu ya wanachuo 
  5. Anahudumia wageni katika Chuo     [       ]

19. Alaa! Kumbe umekuja kwangu leo? Katika sentensi hii neno lililotumika kama kihisishi ni lipi kati ya yafuatayo? _ 

  1. umekuja
  2. kumbe 
  3. leo 
  4. alaa! 
  5. kwangu     [       ]

20. “Kabwela amefiwa na wazazi wake wote wawili.” Je, Kabwela atakuwa na sifa ipi kati ya zifuatazo? ___

  1. Yatima 
  2. Mgane 
  3. Mjane 
  4. Muathirika
  5. Mpweke

21. “Mjomba alikwenda kumuona bibi kijijini.” Ni neno lipi kati ya yafuatayo limetumika kama kielezi katika sentensi hii? ____ 

  1. bibi 
  2. alikwenda 
  3. mjomba 
  4. kijijini
  5. kumuona.

22. “Ninakwenda sokoni.”Sentensi hii ipo katika kauli gani kati ya zifuatazo? ________________________________ 

  1. Tata
  2. Taarifa 
  3. Halisi 
  4. Masharti
  5. Ombi     [       ]

23. Wingi wa sentensi “nimeamua kusoma kwa bidii” ni upi kati ya sentensi zifuatazo? _____ 

  1. Wameamua kusoma kwa bidii 
  2. Umeamua kusoma kwa bidii 
  3. Mmeamua kusoma kwa bidii
  4. Tumeamua kusoma kwa bidii 
  5. Ameamua kusoma kwa bidii     [       ]

24. Methali ipi hutumika kumuonya mtu asiyesikiliza ushauri wa wakubwa? _____

  1. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu 
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu 
  3. Asiyekuwepo na lake halipo. 
  4. Akupaye kisogo sio mwenzako. 
  5. Kidole kimoja hakivunji chawa     [       ]

25. Kukiwa kuna shida ndogo itatuliwe mapema kabla haijawa kubwa. Methali ipi inahusiana na kifungu hicho cha maneno kati ya hizi? ________________________________ 

  1. Hauchi hauchi unakucha 
  2. Mwanzo wa ngoma ni lele 
  3. Usipoziba ufa utajenga ukuta 
  4. Penye miti hapana wajenzi.
  5. Fimbo ya mnyonge ni umoja     [       ]

26. Mashaka ni mtu asiyependa kutunza vitu kwa manufaa ya baadaye. Ni methali ipi kati ya zifuatazo itamsaidia kubadili mwenendo wake? __________________________ 

  1. Akili ni nywele 
  2. Akiba haiozi 
  3. Abwebwaye hujishika 
  4. Adui mpende. 
  5. Ahadi ni deni     [       ]

27. Jogoo washamba ______ Kifungu kipi cha maneno kinaka-milisha kwa usahihi methali hiyo? 

  1. hawiki mjini
  2. huwika mjini 
  3. huwika alfajiri 
  4. huliwa mjini 
  5. hawiki jioni

28. Bute anapenda kudadisi sana ili kuelewa jambo. Methali ipi kati ya zifuatazo inaelezea umuhimu wa tabia ya Bute? _______________________ 

  1. Asiye na bahati habahatishi 
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu 
  3. Asiye na mengi ana machache
  4. Asiyeuliza hana ajifunzalo 
  5. Asiyefahamu urafiki si rafiki     [       ]

29. “Bandu bandu humaliza gogo.” Methali ipi kati ya zifuatazo inafanana na hii? __________ 

  1. Pole pole ndio mwendo. 
  2. Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
  3. Samaki mkunje angali mbichi. 
  4. Chovya chovya humaliza buyu la asali.
  5. Mtaka yote kwa pupa hukosa yote     [       ]

30. Mwalimu Kaze aliwapa wanafunzi wake maswali ya chemshabongo. Nahau “chemshabongo” kama ilivyotumika katika sentensi hii ina maana gani kati ya zifuatazo? ____

  1. Changamsha akili 
  2. Fikiri kwa makini
  3. Sumbua akili 
  4. Fikiri sana 
  5. Amsha ubongo     [       ]

31. Uongozi wa mtaa ulivalia njuga tatizo la uporaji. Nahau “valia njuga” kamailivyotumika katika sentensi hii ina maana gani? _____________ 

  1. Kufuatilia kwa jazba 
  2. Kufuatilia kwa hasira 
  3. Kufuatilia kwa makini 
  4. Kufuatilia kwa siri 
  5. Kufuatilia kwa tahadhar     [       ]

32. Mama alipanga vyombo kabatini. Kinyume cha neno “panga” ni lipi kati ya yafuatayo? __________ 

  1. pangisha
  2. pangusa 
  3. pangua 
  4. panua 
  5. pango     [       ]

33. Babu yangu analima mashamba kwa ustadi. Nomino ipi inatokana na kubadilishwa kwa kitenzi “lima”? ________ 

  1. Limisha
  2. Limiana 
  3. Limika
  4. Mkulima 
  5. Kalime     [       ]

34. Neno linalotokana nakudondosha silabi moja katika neno “sabuni” ni lipi kati ya yafuatayo? ___________________ 

  1. suna 
  2. buni 
  3. bunia 
  4. ibua 
  5. nusa     [       ]

35. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aling’atuka madarakani. Katika sentensi hii, kisawe cha neno “NG’ATUKA” ni kipi kati ya vifuatavyo? _____ 

  1. Kujiuzulu 
  2. Kustaafu 
  3. Fukuzwa kazi
  4. Kustaafishwa 
  5. ng’atua

SEHEMU B: KWA KUTUMIA MANENO YALIYOMO KWENYE KISANDUKU KAMILISHA BARUA IFUATAYO KWAKUJIBU SWALI LA 36 – 40

Baraka Kazingumu, M. Tumaini, Nakutakia utekelezaji mwema, S. L. P 21, YAH. KUPANDISHWA CHEO NA KUBADULISHIWA MAJUKUMU

36.__________

Nachingwea.

04.10.2020

37._________________________

Shule ya Msingi Kisovu,

S. L. P 41,

Namtumbo.

Ndugu,

38._______________________________

Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Napenda kukujulisha kuwa kutokana na utendaji kazi wako mzuri umepandishwa cheo kutoka Mwalimu wa Michezo kuwa Afisa Utamaduni na Michezo wa Wilaya ya Kwetu kuzuri. Hivyo, unatakiwa kuhamia Makao Makuu ya Wilaya punde upatapo barua hii na utawajibika kwa nafasi hiyo.

39._________________________

40._________________________

Masumbuko Tumaini

Mkurugenzi

SEHEMU C: UFAHAMU SOMA KWA MAKINI HABARI IFUATAYO KISHA JIBU SWALI 41 - 45

Kachiku ni kijana mwenye tabia nzuri anayeishi na wazazi wake katika mtaa wa Kibaoni. Alibahatika kuzaliwa peke yake katika familia ya kitajiri. Wazazi wake walimpenda na kumdekeza sana, walimsomesha katika shule nzuri yenye gharama kubwa kwa lengo la kupata elimu bora.

Tabia ya Kachiku ilianza kubadilika kutokana na kuambatana na makundi mabaya shuleni. Kachiku alitumia muda mwingi sana kuzurura mitaani na vijiweni badala ya kusoma. Aliamini kwamba utajiri wa wazazi wake ni nguzo katika maisha yake, akasahau kwamba; “mtegemea cha nduguye hufa maskini. ”Hatimaye, tabia ya Kachiku ikakithiri akaanza kulewa na kuvuta sigara. Unywaji wapombe ulipomkolea akaanza kukwapua vitu vidogovidogo nyumbani kwao ili apate fedha ya kukata maji. Aidha, alikuwa akirudi nyumbani akiwa amelewa chakari. Tabia hiyo haikuwafurahisha wazazi wake. Walijitahidi kumkanyana kumweleza madhara yake lakini alikaidi kama ilivyo ada “sikio la kufa halisikii dawa.”Hakupenda kuwasikiliza wazazi wake na aliona kama wanampotezea muda.

Kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo tabia ya Kachiku ilivyozidi kuwa mbaya. Akaanza kuvunja nyumba za watu na kuiba mali zao. Siku moja, Kachiku na wenzake walikwenda kuiba duka la jirani yao. Kwa bahati walikamatwa na askari aliyekuwa doria. Wazazi wa Kachiku walipigwa na butwaa baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa kijana wao. Kesi ilisikilizwa mahakamani na mwishowe Kachiku alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. 

41. Kichwa cha habari hii kingefaa kuwa kipi? ____________

42. Kutokana na habari uliyoisoma ni tabia gani mbaya alizokuwa nazo Kachiku? Taja mbili.

________________________, _______________________

43. Nini maana ya neno “kanya” kama lilivyotumika katika habari uliyoisoma? _______________________________

44. Kwanini Kachiku alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela? ___________________________________________

45. Unapata funzo gani kutokana na habari uliyoisoma?

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 39

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YAK RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINI MWISHO WA MUHULA

 

KISWAHILI

SEHEMU A SARUFI

Sikiliza kwa makini kifungu cha habari kitakachosomwa na msimamizi kisha jibu maswali 1-5

  1.                Kulingana na kifungu maji yameelezwa kuwa ni
  1.              Hewa
  2.               Mvua
  3.               Uhai
  4.              bahari
  1.                Neno ukame ni sawa na msimu upi?
  1.              Kiangazi
  2.               Vuli
  3.               Kipupwe
  4.              masika
  1.                Ni ukuzaji upi wa maji hutekeleza upanuzi wa uchumi wanchi?
  1.              Kupatia mifugo
  2.               Kusafiria
  3.               Kutolea umeme
  4.              Kuoshea vyombo
  1.                Watu wanaosafirisha maji hawatumii
  1.              Mikokoteni
  2.               Mitungi
  3.               Mifuko
  4.              magari
  1.                Kulingana na kifungu kuna madhehebu ambayo _______ watu wao majini
  1.              huwazalia
  2.               huwaoza
  3.               huwabatiza
  4.              huwauza

 

Sarufi, msamiati na lugha ya kifasihi

6. Fanani aliihakikishia hadhira yake usalama. Maana ya neno fanani ni ____

A. Msikilizaji 

B. Msimuliaji 

C. Mpambe 

D. Mnoko 

E. Mstaarabu

7. Neno lipi kati ya haya lipo katika ngeli ya LI – YA?

A. Ugonjwa 

B. uzima 

C. ufunguo 

D. mbeleko 

E. sherehe

8. Sina nasaba na wewe. Neno lililopigiwa mstari lina maana ya

A. Ukoo 

B. hamu 

C. shauku 

D. dukuduku 

E. haja

9. Watu wengi walihudhuria katika……….. ya harusi ya dada yangu.

A. Kalamu 

B. mahari 

C. Karamu 

D. Mbwembwe 

E. sherehe

10. ni mtu mwenye elimu ya nyota.

A. Mwananyota 

B. Mtabiri 

C. Mnajimu D. Mganga 

E. Bingwa

  1.                     Uliona              baada ya kuingia visiwa vya Pemba? 

A. Ujasiri B. fahali C. hodari D.kuona E. fahari

  1.        Wanafunzi watafanya mtihani wa Kiswahili wiki ijayo, kifungu cha maneno “wiki ijayo” kinaonyesha ___              

A. Kielezi B. kivumishi C. kitenzi D. nomino E. kiwakilishi

  1.                     Katika kitenzi “wanalima” mzizi ni upi?

              

  1.                      Ukila embe bichi utaumia tumbo. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya kivumishi?[ 

A. Idadi B. a__unganifu C. sifa D. kuonyesha E. kumiliki

  1.                     Neno lenye maana sawa au karibu sawa na “maamuma” ni 

A. Marehemu B. mwonevu C. Mjumbe D. Mfuasi E. kati

  1.                     Chakula hiki kina__________________tamu. 

A. Radha B. ladha C. laza D. raza E. latha

  1.                     Mtoto akizaliwa _______________________________________________________

A. Tungesherehekea B. tutafurahi C. tungalifurahi E. furaha D. furahisha

  1.                     Mchanganyiko wa mboga au matunda unaoliwa bila kupikwa huitwa ____________________

A. Mchicha B. nyanya C. kabichi D. saladi E. kachumabri

19. Mpira umegonga mwamba nusura goli liingie. Neno gani linaonesha kitenndwa? [ ]

A. Mwamba B. Nusura C. Goli D. mpra E. liingie

20. Kifaa kinachotumika kuhifadhi kisu huitwa ________________________________[ ]

A. Podo B. ala C. waleti D. rafu E. hori

21. Tegua kitendawili hiki” Maji ya kisima hiki hayawezi kumaliza kiu” [ ]

A. uji B. mate C. Soda D. dafu E. chai

 22. Waliendesha kilimo kwa nguvu zote. Ni nahau ipi inayoendana na melezo haya? [ ]

A. Kufa na kupona B. kufuatana sanjari C. kucheza shere

D. kutia moyo E. kumchimba mtu

23. Mjumbe wetu yu maji wodini. Nini maana ya nahau hii? [ ]

A. Amepona B. Amekaa C. Anacheka D. Amezidiwa E. Buheri wa afya

24. Bura yangu sibadili na rehani. Methali ipi ina maana sawa na hii? 

A. Usiache mbachao kwa msala upitao B. akiba haiozi C. Sikio la kufa halisikii dawa

D. Mfa maji haachi kutapatapa E. Haba na haba hujaza kibaba

25. Majambazi wale walipanga njama zao katika pembe za chaki. Nini maana ya usemi uliopigiwa mstari?              

A. Mahali pa wazi B. Penye haiki ya watu C. Nje ya nyumba

D. Mahali pa siri pasipojulikana E. Mhali pa wazi kuingia

26. Kamilisha methali, baada ya tufani  ______________________________________

A. raha B. huja shwari C. mateso D. mapatano E. huja fujo

27. Mgosi alikuwa na kichwa cha panzi. Msemo “kichwa cha panzi” una maana ipi? 

A. Msikivu sana B. Ana utambuzi C. Msahaulifu sana D. Ana kumbukumbu

E. Mtiifu sana

28. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inapingana na hii, Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu? A. Panya wengi hawachimbi shimo B. Kidole kimoja hakivunji chawa              

  1.                          Palipo na wengi hapaharibiki neno
  2.                          Mkono mmoja hauchinji ng’ombe E. Jifya moja haliinjiki chungu

29. Kamilisha methali hii, “Ukiona zinduna
A. Kuna ajali B. ujue kuna jambo C. ujue kuna fedha D. ambari iko nyuma E. hausimiki

30. Kitendawili, Dume wangu amelilia machungani ______________________________

A. Moto B. radi C. mvua D. jua E. mwezi

31. Mjomba alimpiga___________shangazi ikiwa ni ishara ya upendo. 

A. pasi B. makofi C. viboko D. mguu E. busu

32. Mtu aliyezaliwa nawe kwa baba, kwa mama au kwa wazazi wote wawili utamwitaje?

A. kaka B. binamu C. ndugu D. dada E. jamaa 

33. ____ kwamba wananchi wengi wanajua kusoma na kuandika. 

A. imethihirika B. imezihirika C. imethihirika D. imedhihirika

E. imedhihilika

34. Mahaliambako vita hupiganwa hujulikana kama ______________________________

A. dimba B. medani C. ulingo D. uga E. uzio

35. Mafuta yanayotokana na wanyama kama ng’ombe au ngamia ambayo hutumika kupikia huitwa __ 

        A. mtindi B. siagi C. jibini D. mgando E. samli

SEHEMU YA B

UTUNGAJI

Panga sentensi zifuatazo katika mtiririko unaofaa kwa kuzipa herufi A to E

36. Mwalimu na wanafunzi wenzangu walinipongeza sana.

37. Mwezi uliopita tulifanya jaribio la Kiswahili.

38. Sasa naendelea kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa taifa mwezi Septemba.

39. Baada ya siku moja, matokeo ya jaribio hilo yalitoka.

40. Mimi nilifanikiwa kupata alama tisini na kuwa wa kwanza katika darasa.

SEHEMU C: UFAHAMU

Soma habari ifuatayo, kasha jibu maswali.

Waandishi mashuhuri ambao walikuwa hodari kwa kufikiri na kutunga mambo yenye tija, ilipofika safari kwenda kusiko na rejea basi halikuweza kuwa na saburi wote wamekwenda zao. Walikuwa watu wenye kupendwa na walipenda kuwafadhili wenzao. Watu hawa walipendwa kwa mapenzi ya ajabu mfano hakuna. Imebaki historia maana kurejea hawawezi hata tulie vilio na machozi ya damu hawawezi kurudi watu hao. Walitenda mambo kwa hekima zote katika uhai wao, basi wakawa wenye kuvuma kwa vyeo na sifa zao. Wote wamezama na zimebaki sifa zao.

MASWALI

  1. Watu ambao wanazungumzia kwenye habari walikuwa akina nani?_____________________
  2. Mwandishi wa habari hii ameelekeza kuwa, watu wanazungumzia wamekwenda

wapi?_____________________________________________________________

  1. Nini maana ya neno saburi kama ilivyotumika kwenye habari? _______________________
  2. Kwanini mwandishi anasema watu hai walikuwa hodari?
  3. Mwandishi anaposema wote wamezama ana maanisha nini?

 

KIFUNGU CHA SWALI LA KWANZA

Maji ni uhai. Maji huhitajika katika maisha yetu ya kila siku. Tunahitaji maji ya kunywa, kupika , kuoshea na kupatia mifugo yetu

Maji ni muhimu katika kilimo. Mimea haiwezi kustawi bila maji. Maeneo ya nchi ambayo hayana mvua au mito hayavutii watu wengi kuishi humo. Wenyeji wa sehemu hizo hukabiliwa na ukame miaka nenda miaka rudi. Baadhi yao hufa kwa njaa. Wengine hukonda na kuwa wembamba kama sindano kwa kukosa lishe bora

Viwanda navyo huhitaji maji ili kuendeleza shughuli zao. Nguvu za umeme anghalabu hutolewa kwenye mianguko ya maji. Bila umeme nchi haiwezi ikastawi ipasavyo kiuchumi.

Katika nchi imani za kidini, kuna madhehebu ambayo hutumia maji kubatiza waumini wao. Watu wengi huamini ni baraka kutoka kwa mungu.

Watu wengi huuza maji na kujipatia riziki zao. Wao hutumia mitungi, mikokoteni na hata magari kusafirisha maji

Maji ni muhimu katika nyanja za usafiri . kuna maeneo makubwa ya nchi yenye maji pakee. Haya huitwa bahari abiria wanakosafiri majini hutumia meli kwa hivyo matumizi ya maji ni chungu nzima. Kwa kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame hatuna budi kuhifadhi maji na pia kutunza sehemu yanakotoka ili yaendelee kutufaa.

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 31

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021

KISWAHILI – DARASA LA SABA

FOMATI MPYA

MUDA1:30 MASAA MACHI 2021

JINA …………………………...SHULE ………………………...

SEHEMU A SARUFI

Chagua jibu sahihi

  1. “Mwanamuziki Hodari aliimba nyimbo vizuri” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? (a) hodari (b) aliimba (c) mwanamuziki (d) vizuri (e) Nyimbo.
  1. Neno MBWA lina silabi ngapi? (a) nne (b) mbili (c) tatu (d) moja (e) sifuri.
  1. Kisawe cha neno shaibu ni…………………(a) barabara (b) baneti (c) kigori (d) ajuza (e) buda.
  1. Katika neno “Wanifuata” kiambishi kinachoonesha njeo ni (a) –wa- (b) –fuat-

(c)-ni-(d)-na-(e)-a-

  1. Kipi kinyume cha neno aghalabu?
  1. Mara nyingi (b) mara kwa mara (c) nadra (d) muda wote (e) kila wakati.
  1. Mtoto wa nzige anaitwa kimato. Mtoto wa simba anaitwaje?
  1. Shibli (b) Kitungule (c) Ndama (d) Mwanasimba (e) Kinda
  1. Kinyume cha neno ughaibuni ni (a) nchi jirani (b) nchi za mbali
  1. magharibi (d)nyumbani (e) mashariki
  1. Wewe subiri. Neno wewe lipo katika nafsi ya (a) kwanza umoja (b) pili wingi
  1. Pili Umoja (d) tatu wingi (e) tatu umoja
  1. Alimua kuweka ________ ili kulinda nyumba yake baada ya kuibiwa (a) bawaba
  1. Bawabu (c) ukuta (d) Mbwa E.)Mgambo
  1. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatao (a) senge’nge (b) wigo (c) ukuta (d) ukingo (e) barabara
  1. Mwanafunzi anapika ugali. Mzizi wa neno anapika ni(a)ana(b)pika(c)pik (d) anap
  1. “Ukifanya vizuri utapongezwa,” sentensi hii ni ya aina gani? (a) kutenda
  1. Shurutia (d)Kutendeana (e) kutendwa
  1. Wanyama wengi wanaishi msituni. Neno mstuni ni……… (a) kitenzi (b) kielezi
  1. kivumishi (d)kiwakilishi (e) kiunganishi
  1. “Uji huu una sukari na maziwa”. Ukanushi wa kauli hii ni upi?
  1. Uji huo hauna sukari ila maziwa
  2. Uji huu hauna sukari wala maziwa
  3. Uji huo hauna sukari bila maziwa
  4. Uji huu sukari bila maziwa
  5. Uji huu hauna lakini una maziwa
  1. Neno kitongoji lina kosonati ngapi? (a) Moja (b) Mbili (c) Tano (d) Tatu (e) Kumi
  1. Neno lipi kati ya yafuatayo halilandani na mengine? (a) kuonja (b) kuona

(c)kunusa (d) kusikia (e) kutoa jasho

  1. Alipofika Shuleni aliwakuta Wanafunzi wanaimba nyimbo vizuri. Sentensi

hii inahusika na ngeli ipi? (a) U-YA (b) LI-YAK (c) A-WA (d) U-ZI (e) KI-VI

  1. Mahindi, maharage, ufuta, michungwa, migomba na mihogo kwa neno moja ni; (a) mimea

(b) nyakula (c) matunda (d) mboga (e) Miche

19. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana saw ana neno “zuzu”

(a) mjanja (b) Mpole (c) mjinga (d) mzubafu (e) Mzururaji

20. Kisawe cha neno chumvi ni _____ (a) (Mbogo) (b) Munyu (c) Saladi

(d) Chachanda (e) Mbogamboga

SEHEMU B

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

21. Msemo "kubarizi" maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya .

  1. Sherehe
  2. mkutano
  3. mazungumzo ya kawaida
  4. burudani
  5. chakula cha pamoja

22. Methali isemayo "Kila mtoto na koja lake" ina maana gani?

  1. Kila binadamu ana mapungufu yake.
  2. Kila mtoto ana matatizo yake.
  3. Kila mtoto ana mapungufu yake.
  4. Kila mtoto ana wazazi wake.
  5. Kila binadamu ana tabia yake.

23. Nahau isemayo "kuvishwa kilemba cha ukoka" ina maana gani?

  1. Kupewa sifa unazostahili
  2. Kupewa sifa mbaya
  3. Kupewa sifa nyingi
  4. Kupewa sifa chache
  5. Kupewa sifa usizostahili

24. Tegua kitendawili kifuatacho: "Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji."

  1. Kikombe
  2. Kata
  3. Kinywa
  4. Kibatari
  5. Mtungi

25. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haifanani na zingine?

  1. Mtegemea nundu haachi kunona.
  2. Nazi haishindani na jiwe.
  3. Mlinzi wa kisima hafi kiu.
  4. Mchumia juani hulia kivulini.
  5. Baada ya dhiki faraja.

26. Mwamba ngoma .. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hiyo?

  1. hualika watu wengi
  2. hufanya maandalizi mengi
  3. huimba nyimbo nyingi
  4. ngozi huvutia kwake
  5. hucheza na jamaa zake

27.Ni methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza ushirikiano katika jamii?

  1. Chanda chema huvikwa pete
  2. Mchumajanga hula na wa kwao
  3. Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu
  4. Mwenda pole hajikwai
  5. Wapishi wengi huharibu mchuzi

28. "Uzururaji umepigwa marufuku".Nahau umepigwa marufuku ina maaña gani?

  1. Umezoeleka
  2. Umepigwa winda
  3. Umepigwa konde
  4. Umekithifi
  5. Umekatazwa

29. "Mwenye nguvu Neno linakamilisha methali hii?

  1. mfunge
  2. usimkamate
  3. mkimbie
  4. usimpigie
  5. mpishe

30. "Haba na haba hujaza kibaba" Methali hii inatoa funzo gani?

  1. Umuhimu wa kupima vitu
  2. Tunajiwekea akiba
  3. Vitu hupimwa na kibaba tu
  4. Tunapawa kupima vibaba
  5. Kibaba hujaza vitu.

SEHEMU D

USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa Kuweka kivuli katika herufi ya jibu.

Mtu kujitegemea, huwajambo Ia lazima,

Usipende subiria, kusaidiwa daima,

Huwezi kuendelea, ndugu usipojituma,

Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema, Fedheha kuombaomba, takuwa mtu wa nyuma, Hutakuja kujigamba, ukikudharau umma. Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kazi mtu usidhani, sharti niya kusoma,

Ya kuleta ofisini, na kuhesabu ndarama,

Waweza kwenda shambani, ushikejembe kulima, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima,

Pengine uitwe mwizi, umezoea dhuluma, Wajapo wapelelezi, ndiwe watakuandama, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

31. Katika shairi ulilosoma neno "ndarama" lina maana ipi?

  1. Mali
  2. Pesa
  3. Gharama
  4. Amana
  5. Thamani

32. Kisawe cha neno "taadhima" ni kipi?

  1. Heshima
  2. Taashira
  3. Dhamiri
  4. Dhima
  5. Dhamana

33. Ujumbe unaopatikana katika shairi hili unaweza kuwasilishwa kwa methali ipi kati ya zifutazo? ........

  1. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi
  2. Mchagua jembe si mkulima
  3. Mkulima hasahau jembe kiserema
  4. Mkulima halaumu jembe lake
  5. Kilimia kikizama kwa jua huibuka

34. Katika shairi ulilosoma kituo bahari ni kipi?

  1. Mtu kujitegemea, huwa jambo la lazima.
  2. Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema.
  3. Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima.
  4. Waweza kwenda shambani, ushike jembe kulima
  5. Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

35. Katika shairi ulilosoma nusu mstari una mizani ngapi?

  1. Nane
  2. Mbili
  3. Tatu
  4. Nne
  5. Kumi na tano

SEHEMU D: UTUNGAJI

Zipange Sentensi kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E ili kupata mantiki

  1. Baada ya kusubiri kwa nusu saa, basi liliwasili na nikapanda kwenda bunda
  1. Abiria wote walishuka kutoka kwenye gari moshi
  1. Lilipowasili mjini mwanza, gari moshi lilisimama taratibu na kutangaza kuwa hapo ndio ulikua mwisho wa safari yake.
  1. Nami nilishuka na kwenda moja kwa moja hadi kituo cha mabasi
  1. Mimi na abiria wenzangu tulisafiri kwa amani na kufika bunda salama jioni.

SEHEMU E: UFAHAMU

Soma habari ifuatayo kasha jibu maswali yafuatayo kwa kujaza nafasi

Watanzania hatuna budi kujivunia amani na utulivu tulivyonavyo. Angalia majirani zetu wanavyozikimbia Nchi zao kwa sababu ya vita vya mara kwa mara. Kutokana na Amani tunapiga hatua katika sekta za kilimo na uwekezaji. Wakulima wamepiga hatua katika kutumia jembe la kukokotwa na wanyama, matumizi ya mbolea na mbegu bora. Nasikitishwa na migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi. Hebu tujiulize chanzo ni nini? Mimi nashauri haki na wajibu viende sambamba ili kuleta ufanisi katika kazi, hatimayee kuepuka migogoro katika Jamii yetu ili tuendelee kuwa na amani daima.

MASWALI

  1. Mwandishi wa habari hii anawapongeza watu wake kujivunia nini? ___________
  1. Majirani zake Mwandishi wanakimbia Nchi zao kutokana na kitu gani?_________
  1. Mambo gani yakiwa sawiya katika Jamii yataleta ufanisi katika kazi? __________
  1. Sekta zipi zimesonga mbele kutokana na utulivu uliopo Nchini? ______________
  1. Watu wanaokimbia machafuko katika Nchi zao na kwenda Nchi jirani wanaitwaje? ________________

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 22

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YAK RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINI YAAWALI DARASA LA VII JAN 2020

KISWAHILI

SEHEMU A SARUFI

Chagua jibu sahihi

  1. Wao ni watiifu sana kwa Walimu wao. Neno Watiifu ni aina gani ya maneno (a) Kitendwa (b) Kiwakilishi (c) Nomino (d) Kitenzi (e) Kivumishi
  1. Neno lipi linakamilisha Sentensi isemayo; “Humo ______________ alimoingia yule nyoka  (a) ndiye (b) ndipo (c) ndiyo (d) ndimo (e) ndiko
  1. Ngeli ya umoja ya neno ‘’Ugonjwa’’ ni ipi @ K (b) I (c) Z (d) Y (e) U
  1. Katika neno “Wanifuata”  kiambishi kinachoonesha njeo ni (a) –wa- (b) –fuat-

          (c)-ni-(d)-na-(e)-a-

  1. Neno  “cherekochereko” limeundwa na silabi ngapi?
  1. Nane (b) kumi na moja (c) saba (d) mbili (e) sita
  1. Mtoto wa nzige anaitwa kimato. Mtoto wa simba anaitwaje?
  1. Shibli (b) Kitungule (c) Ndama (d) Mwanasimba (e) Kinda
  1. Loo! Amefeli mtihani. Neno loo! limetumika kama (a) kihisishi (b) kiwasilishi
  1. kielezi (d)kitenzi (e)Nomino
  1. Wewe subiri. Neno wewe lipo katika nafsi ya (a) kwanza umoja (b) pili wingi
  1. Pili Umoja (d) tatu wingi (e) tatu umoja
  1. Alimua kuweka ________ ili kulinda nyumba yake baada ya kuibiwa (a) bawaba
  1. Bawabu (c) ukuta (d) Mbwa E.)Mgambo
  1. Neno kuliwaza lina maana sawa na (a) kufariji (b) kutuliza (c) kufikiria (d) kuota (e) kuhuzunika
  1. Mwanafunzi anapika ugali. Mzizi wa neno anapika ni(a)ana(b)pika(c)pik (d) anap
  1. Nitakupa sasa hivi kwa sababu baadaye sitakuwa na ________ wa kuja (a) saa
  1. Fursa (d)Wasaa (e) Nafasi
  1. Wanyama wengi wanaishi msituni.  Neno mstuni ni……… (a) kitenzi (b) kielezi
  1. kivumishi (d)kiwakilishi (e) kiunganishi
  1. Hadi sasa hakuna Mwanafunzi ____aliyeshindwa kufanya Mtihani wa Taifa (a)yoyote (b) wowote (c) yeyote (d) wowote
  1. Neno kitongoji lina kosonati ngapi? (a) Moja (b) Mbili (c) Tano (d) Tatu (e) Kumi
  1. Watalii wengi hufika Tanzania ili ____Mbuga za wanyama (a) kuzuru (b) kuthuru

          (c)kudhuru (d) kufuru (e) kudhulu

  1. Alipofika Shuleni aliwakuta Wanafunzi wanaimba nyimbo vizuri.  Sentensi

hii inahusika na ngeli ipi? (a) U-YA (b) LI-YAK (c) A-WA (d) U-ZI (e) KI-VI

  1. ______ni mtu ambaye hajawahi kuowa au kuolewa maishani mwake. (a) Ajuza

(b) Mseja (c) Shaibu (d) Buda (e) Mzee

      19. Yule Bibi kizee ameishi miaka mia moja. Miaka mia moja ni sawa na __

             (a) Karne (b) Muongo (c) Milele (d) Milenia (e) Daima

       20. Kisawe cha neno chumvi ni _____ (a) (Mbogo) (b) Munyu (c) Saladi 

             (d) Chachanda (e) Mbogamboga

SEHEMU B

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

  1. Methali ipi kati yak hizi ni tofauti na nyingine? (a) Mwendapole hajikwai (b) Kawia ufike (c) Ngojangoja huumiza matumbo (d) Harakaharaka haina baraka
  1. polepole ndio mwendo
  1. Ubwabwa wa mwana mtamu ni……… (a) Usingizi (b) Uvivu (c) Mtamu (d) Mafuta e) Wali
  2. Bibi kizee chapepeta mafuta. Jibu la kitendawili hiki ni……. (a) Alizeti (b) Mpunga (c) Pamba (d) Chikichi (e) Uwele
  1. Nahau ipi ina maana sahihi na ile isemayo sina hali……. (a) kufa kishujaa

(b) Kupoteza maisha (c) Sina mbele wala nyuma (d) Machozi kulenga (e) Tajiri

     25. “Kata shauri” ina maana ya __ (a) kata kamba (b) kata macho (c) Amua (d) jihoji   

            (e) fikiri

  1. Malizia methali hii “kutoa ni moyo (a) si ujinga (b) si ulemavu (c) si utajiri (d) si uchoyo (e) si ulevi
  1. “Ba funua ba funika” Jibu la kitendawili hiki ni (a) kulima (b) kula (c) kucheza

           (d) kutembea (e) kula

  1. Nimepigwa faini kosa silijui (a) kujikwaa (b) Mwizi (c) kutembea (d) Mwalimu

(e)Mtoto

  1. Jifya moja ______ Chungu. Malizia methali hii. (a) tofali (b) umeme (c)jiko la

            mkaa (d) haliinjiki  e.)Halikati

  1. Toa maana ya kitendawili hiki “Ngozi ndani nyama nje” (a) Kobe (b) Embe
  1. Papai (d) Firigisi (e) Nanasi

SEHEMU C: USHAIRI

Soma ushair kasha jibu maswali

Mtima imenikuna, kwa dafina teletele,

Samaki wa kumimina, change,sato, kolekole,

Ziwa la kirefu kina, kina kirefu milele,

Thamani ya Nchi yangu, haimithiliki kamwe.

Kamwe haimithiliki, ukitazama Bahari

Bandari hazipimiki, mimi naona fahari

Uvuvi haushikiki, pwani yote itayari

Nani bado haelewi? Ajikune nimuone.

  1. Nini maana ya neno “mtima” kama lilivyotumika katika shairi (a) moyo

(b) kichwa (c) chanda (d) akili (e) watu

  1. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi? (a) 2 (b) 3 (c)4 (d) 16 (e) 8
  1. Vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa pili ni (a) ki,ki (b) me,no (c) ki, li

d) ki, ri (e) wi,ne

  1. Samaki aliowataja mshairi ni _____(a) kolekole, konbe, sato

(b) sato,sangara,kolekole (c) kolekole, sato, change (d) changu, sato, perege 

(e) hakuna jibu

     35. Mstari mmoja wa kila shairi huitwa (a) mshororo (b) vina (c) mizani (d) mkarara, 

           (e) kitoshelezi

SEHEMU D: UTUNGAJI

Zipange Sentensi kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E ili kupata mantiki

  1. Akasikia sauti kwa mbali akimuita “UUU”
  1. Alipofika katikati ya msitu akasoma ile aya kwa utulivu
  1. Alipokwisha pata maelezo yake akaondoka hadi msituni
  1. Mweka nadhiri akasema “Njoo”!
  1. Alipomaliza akapaza sauti “Shetani ee”

SEHEMU E: UFAHAMU

Soma habari ifuatayo kasha jibu maswali yafuatayo kwa kujaza nafasi

Watanzania hatuna budi kujivunia amani na utulivu tulivyonavyo.  Angalia majirani zetu wanavyozikimbia Nchi zao kwa sababu ya vita vya mara kwa mara. Kutokana na Amani tunapiga hatua katika sekta za kilimo na uwekezaji. Wakulima wamepiga hatua katika kutumia jembe la kukokotwa na wanyama, matumizi ya mbolea na mbegu bora.  Nasikitishwa na migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi.  Hebu tujiulize chanzo ni nini? Mimi nashauri haki na wajibu viende sambamba ili kuleta ufanisi katika kazi, hatimayee kuepuka migogoro katika Jamii yetu ili tuendelee kuwa na amani daima.

MASWALI

  1. Mwandishi wa habari hii anawapongeza watu wake kujivunia nini? ___________
  1. Majirani zake Mwandishi wanakimbia Nchi zao kutokana na kitu gani?_________
  1. Mambo gani yakiwa sawiya katika Jamii yataleta ufanisi katika kazi? __________
  1. Sekta zipi zimesonga mbele kutokana na utulivu uliopo Nchini? ______________
  1. Watu wanaokimbia machafuko katika Nchi zao na kwenda Nchi jirani wanaitwaje? ________________

MUONGOZO WA MAJIBU YA SOMO LA KISWAHILI: DARASA LA SABA 2021

1.

E

26

C

2.

D

27

D

3.

E

28

A

4.

C

29

D

5.

E

30

D

6.

A

31

A

7.

A

32

A

8.

C

33

D

9.

B

34

B

10.

A

35

A

11.

C

36

D

12.

D

37

B

13

B

38

A

14

C

39

E

15

C

40

C

16

A

41

AMANI NA UTULIVU

17

C

42

VITA VYA MARA KWA MARA

18

B

43

HAKI NA WAJIBU

19

A

44

KILIMO NA UWEKEZAJI

20

B

45

WAKIMBIZI

21

C

22

A

23

A

24

C

25

C

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 19


THE PRESIDENT’S OFFICE

MINISTRY OF EDUCATION, LOCAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

KISWAHILI- PRE-NATIONAL EXAMINATION-SEPT

STD SEVEN

TIME: 1.30 HRS                                                                                           2020

NAME:_______________________________________CLASS:___________

          INSTRUCTIONS

  1. This paper consists of three sections A, B,C and D
  2. Answer all questions in all sections
  3. All answers should be written in spaces provided
  4. Ensure clarity in your work

 

SEHEMU A: SARUFI Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufl ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia

1. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya haya

  1. Chungwa
  2.  Embe
  3. Ndizi
  4. Nanasi
  5.  Mgomba

2.  Mto Ruvu umefurika mwaka huu. Katika sentensi hii, maneno "mwaka huu" ni ya aina gani?

  1. Nomino image
  2.  Vitenzi
  3. Vivumishi
  4. Vielezi
  5. Viwakilishi

3."Mimi sitakuja" Sentensi hii iko katika kauli gani?

  1. Kanushi
  2. Ombi
  3. Swali 
  4.  Taarifa 
  5. Halisi 

4.Mama mdogo amepika ugali mwingi". Maneno gani ni vivumishia sentensi hii?

  1. Mdogo na mwingi
  1. Mama na mdogo
  2. Uglai na mwingi  image
  1. Mdogo na amepika 
  2. Amepika na ugali

5.       "Wakulima wamehamisha mizinga ya nyuki kutoka mashambani mwao. "Umoja wa sentensi hii ni upi?

  1.  Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani mwao. 
  2.  Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwake
  3. Mkulima amehamisha mizinga ya nyuki kutoka shambani imagemwake.
  4. Mkulima amehamisha mzinga wa nyuki kutoka shambani mwao.
  5.  Mkulima amehamisha mzinga ya nyuki kutoka shambani mwake.

6.      Wingi wa sentensi "Mbuzi wamepotea" ni upi?

  1. Mbuzi zetu zimepotea
  2. Mbuzi yetu zimepotea
  3. Mbuzi wetu wamepotea 
  4.  Mbuzi zetu wamepotea
  5. Mbuzi yetu wamepotea.

7.      "Wanafunzi kenda walikwenda ziara nchini Kenya".neno wa ni aina gani ya neno?

  1. imageKivumishi image
  2. Kiwakilishi
  3. Kielezi 
  4.  Kitenzi
  5. Nomino.

8.      Ashura anacheza mpira wa miguu vizuri.katika sentensi hii,neno lipi limetumika kama kielezi? image

  1. Anacheza
  2.  Mpira
  3. Vizuri
  4. Ashura
  5. Wa mguu.

9. Mtu anayetafsiri ana kwa ana katika lugha moja kwenda lugha nyingine huitwaje? 

  1. Msuluhishi
  2. Mpatanishi
  3. Mkalimani
  4.  Mfafanuzi
  5. Mhubiri

10. "Sote tunafanya mtihani darasani". "darasani" limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Kivumishi image
  3. Kitenzi
  4. Kiwakilishi 
  5.  Nomino

11.      "Tulicheza ngoma na kuimba usiku kucha.” Katika sentensi hii watenda ni nafsi ipi?

  1. Ya tatu wingi 
  2. Ya pili wingi
  3.  Yapili umoja
  4. Ya tatu umoja 
  5. Ya kwanza wingi.

12.      ”Utundu wake ulimfanya ajulikane shuleni.” Neno "Utundu” limetumika kama aina gani

neno? 

  1. Kivumishi  
  2.  Nomino
  3.  Kiwakilishi
  4.  Kitenzi  
  5. Kielezi.

13.      "Mwanamuziki hodari aliimba nyimbo vizuri.” Kielezi katika sentensi hii ni kipi? ........

  1. Hodari 
  2.  Aliimba 
  3. Mwanamuziki
  4. Nyimbo  
  5. Vizuri

14.      "Mgeni aliondoka alikofikia.............kuaga.” Kifungu kipi cha maneno kinachokamilishE sentensi hiyo kwa usahihi?

  1. licha ya 
  2. pasi ya 
  3. bila kwa 
  4.  bila ya   
  5.  bila na

15.      Neno moja linalojumuisha herufi "a, e, i, o na u” ni lipi? 

  1. Silabi   
  2.  Konsonanti   
  3. Mwambatano
  4.  Kiambishi 
  5. Irabu.

16. "Mtoto ametengeneza toroli Ia mti." Wingi wa sentensi hii ni upi?

  1.  Watoto wametengeneza toroli za miti
  2.  Watoto wametengeneza matoroli ya mti
  3.  Watoto ametengeneza matoroli ya miti
  4.  Watoto wametengeneza toroli za mti
  5.  Watoto wametengeneza matoroli ya miti

17. "Muda mfupi atakuwa anaingia uwanjani." Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1. Uliopo
  2. Uliopita
  3. Wa mazoea
  4. Ujao
  5. Timilifu

18. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?

  1. Fikiria
  2. Dodosa
  3. Uliza
  4. Hoji
  5. Saili

19. Juma aliondoka hivi punde. Maneno "hivi punde" yana maana ipi?

  1. Haraka
  2. Muda mrefu
  3. Karibuni
  4. Kwa pupa
  5. Kwa haraka

20. Neno lipi ni kisawe cha neno adili?

  1. Ujinga
  2. Wema
  3. Uovu
  4. Ujasiri
  5. Ukatili

SEHEMU B

LUCHA YA KIFASIHI

Katika swali la 21 — 30 andika katika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

21. "Mwanzo wa ngoma ni lele.” Methali inayofanana na hii kati ya hizi zifutazo ni ipi?

  1.  Dawa ya moto ni moto 
  2. Dalili ya mvua ni mawingu
  3.  Dira ya binadamu ni kichwa 
  4.  Dawa ya jibu ni kulipasua 
  5.  Mtoto wa nyoka ni nyoka

22. "Akutendaye mtende usimche akutendaye.” Methali hii inatoa funzo gani?

  1.  Mwovu akomeshwe kwa adhabu kali
  2.  Akufanyiae maovu usimche 
  3. Mwovu akwepwe kwa kutenda.
  4. Anayekutendea usilipize kisasi 
  5. Mwovu akwepwe kwa kutendwa

23. "Uzuri wa mkakasi ndani .........” Ni kifungu kipi kati ya vifuatavyo kinakamilisha methali hiyo?

  1. kuna mti laini 
  2. kipande cha mdalasini
  3. kipande cha mti 
  4. ni mti mkavu 
  5. kipande laini.

24. Msemo upi kati ya ifuatayo unakamilisha sentensi, "Kinjekitile alijaribu lakini baadaye hakuitekeleza.”

  1. Kuweka hadhari 
  2. kuweka nadhiri
  3. kuweka hadhira 
  4. kuweka nadharia
  5. kuweka nadhari

25. Tegua kitendawili kisemacho, " Atembeapo kila mara huringa hata kama kuna adui.”

  1.  Bata 
  2. Konokono 
  3.  Kobe
  4.  Kanga 
  5.  Kinyonga

26. "Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake." Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana save na hiyo?

  1.  Pema usipopema ukipema si pema tena
  2.  Kizuri hakikosi ila
  3.  Mtu siri kusema na moyo wake
  4.  Nyumba usiyoilalia ndani hujui ila yake
  5. Pilipili usiyoila yakuwashia nini

27. "Nina mwanangu mweupe nikimtia maji hufa." Kitendawili hicho kina maana ipi?

  1.  Maziwa 
  2.  Tui la nazi 
  3.  Majivu 
  4.  Barafu 
  5. E. Karatasi

28 Bwana mkubwa amelala ndani lakini ndevu zipo nje zapepea." Jibu sahihi la kitendawili hiki ni lipi?

  1. . Ulezi 
  2. . Mpunga 
  3. . Ngano 
  4. . Mahindi 
  5. . Mtama

29. "Kazi mbaya si mchezo mwema." Methali inayofanana na methali hiyo ni ipi?

  1.  Hewala haigombi.
  2.  Mchezea tope humrukia.
  3.  Heri kuwa mbichi kuliko kuungua. 
  4. Hucheka kovu asiyekuwa na jeraha.
  5. Hukunyima tonge, hakunyimi neno.

30. Msemo usemao, "kushikwa sikio" una maana ipi?

  1.  Kusemwa 
  2. Kunongonezwa 
  3.  Kuelezwa
  4. Kusengenywa 
  5. Kuonywa

SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kifungu cha habari na kishajibu maswaliyanayofuata:

Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi. Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza, ikifuatiwa na chakula. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya viumbe wengine yasingewezekana. Kila mtu anaelewa umuhimu wa maji katika maisha. Maji yanatawala maisha kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya viumbe kama vile samaki, mamba, kasa, konokono, nyangumi na wengineo maskani yao ni majini, hivyo maji yakikosekana viumbe hao huweza kuaga dunia.

Binadamu anatumia maji kwa shughuli mbalimbali. Shughuli hizo ni pamoja na kupikia, kufulia, kusafishia vyombo, kuoga na kunywa. Katika sehemu nyingi za nchi yetu watu hutumia maji kwa kumwagilia bustani za mboga, maua na miti. Katika maeneo yenye mito mikubwa na maziwa maji yake hutumika kwa kumwagilia mashamba kama yale ya mpunga na mahindi. Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwa sababu mkulima anakuwa na uhakika wa kuvuna.

Maji ya mvua huwezesha watu kulima na kupanda mazao ya chakula na ya biashara. Hivyo zipo sehemu ambazo wakulima hulima kilimo cha umwagiliaji lakini sehemu kubwa ya wakulima hutegemea kilimo cha mvua.

Kwa ujumla maji yawe ya mvua au yanayotokana na mito au maziwa yana umuhimu mkubwa mno kwa binadamu kama walivyosema wahenga maji ni uhai, hivyo inashauriwa kwamba ni muhimu kwa kila mtu kunyvva maji safi na salama ili kulinda siha zetu.

MASWALI

31.Vitu vitatu muhimu vinavyomwezesha binadamu kuishi ni vipi?

  1. Hewa, chakula na nyumba 
  2. Hewa, maji ma chakula
  3.  Maji ushauri na hewa 
  4. Maji, hewa na mvua
  5. Chakula, mvua na hewa

32.Wakulima wengi kama ilivyoelezwa katika habari hii hulima kilimo kinachotegemea nini?

  1.  Mito 
  2.  Umwagiliaji 
  3. Mvua
  4. Mabwawa 
  5.  Maziwa

33. Kiumbe yupi kati ya wafuatao halandani na wenzie?

  1.  Kima 
  2.  Mamba
  3. Nyangumi
  4. Kasa
  5. Samaki

34.Kilimo cha umwagiliaji kina sifa gani kubwa?

  1.  Uvunaji upo dhahiri 
  2. Kinatumia maji ya maziwa makubwa
  3. Kinatumia maji yaliyohifadhiwa 
  4. Mazao hayapati magonjwa 
  5. Kinalimika majira yoyote

35.Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani?

  1. Afya njeme
  2. Sifa njema
  3. Maisha mema
  4. Tabia njema
  5. Kinywa safi

36. "Kuaga dunia" ni msemo wenye maana gani?

  1. Kuzirai 
  2. Kuzimu
  3. Kulala fofofo
  4. Kufariki 
  5. Kufia mbali

37. Ni kwanini mtunzi wa habari hii anashauri watu kunywa maji safi na salama?

  1.  Ili kuondokana na kiu 
  2.  Ili kulinda vinywa vyetu
  3.  Ili kuburudisha mwili 
  4.  Ili kuondokana na kichocho 
  5.  Ili kulinda afya zetu

38.Neno "maskani" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?

  1.  Nyumba 
  2.  Makao 
  3.  Maisha 
  4.  Mahitaji 
  5.  Shughuli

39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?

  1.  Hewa ni muhimu 
  2.  Maji ni uhai
  3.  Maji salama 
  4.  Hewa na chakula
  5.  Siha bora

40.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?

  1.  Hewa ni muhimu 
  2.  Maji ni uhai
  3.  Maji salama 
  4.  Hewa na chakula
  5.  Siha bora

 

Katika swali la 41-45 andika jibu kwa kifupi kwenye nafasi uliyopewa Soma habari hii kwa umakini kisha ujibu maswali

Wakati elimu haijakua watu hawakujua kuhusu dunia yetu. Waliokuwepo waliamini kuwa dunia ni tambarare kama image meza, wakiamini kuwa mtu anaweza kutembea hadi akafika mwisho wa dunia na kuanguka kwenye shimo kubwa. Wengine waliamini kuwa kama ungeendelea kWenda mwishowe ungegusa mbingu. imageBaadae wataalamu       wa anga walithibitisha kuwa dunia la ina umbo duara kama tufe.

MASWALI

Jibu maswali haya kwa umakini.

41.      Zamani watu waliamini kuwa dunia ni tambarare kama 

42.   Wataalamu wa mambo ya anga walithibitisha kuwa dunia ina

43. Watu wengi waliamini kuwa mtu imageangeendelea kwenda mwishowe angegusa?

44.      Wengine waliamini kuwa mtu anaweza kutembea hadi akafika mwisho wa Dunia na kuanguka

kwenye 

45.      image Kichwa cha habari hi kingefaa kiwe

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 12

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KISWAHILI- MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA

DARASA LA SABA

MUDA: 1.30                                                        DARASA LA VII

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina kurasa nne zenye maandishi yenye sehemu A,B, C,D na E zenye maswali arobaini na tano (45).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
  3. Kumbuka kuandika majina yako, na shule yako kwenye karatasi ya kujibia.
  4. Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
  5. Tumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi kwa maswali yote uliyopewa.

SEHEMU : A SARUFI

Chagua herufi ya jibu sahihi kisha uiandike kwenye karatasi ya kujibia uliyopewa

1. Wingi wa neon uteo ni nini?

  1. Mateo
  2. Teo
  3. Uteo
  4. Mauteo
  5. Lungo.

2. Kitenzi “anapigwa” kipo katika kauli gani?

  1. Kutenda
  2. Kutendwa
  3. Kutendewa
  4. Kutendeka
  5. Kutendesha

3. Wingi wa neon “paka” ni ipi?

  1. Mipaka
  2. Paka
  3. Mapaka
  4. Vipaka
  5. Wapaka.

4. Kisawe cha neon bahati ni kipi kati ya maneno yafuatayo?

  1. Tunu
  2. Sudi
  3. Shani
  4. Hiba
  5. Hidaya

5. Ni neon lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?

  1. Fikiri
  2. Dodosa
  3. Uliza
  4. Hoji
  5. Saili

6. Juma aliondoka hivi punde; maneno “hivi punde” yanamaana gani?

  1. Haraka
  2. Muda mrefu
  3. Karibuni
  4. Kwa pupa
  5. Kwa haraka

7. Sweta langu limeshonwa na fundi mzoefu, “mzoefu” ni aina gani ya neon?

  1. Kielezi
  2. Kivumishi
  3. Kiunganishi
  4. Nomino
  5. Kitenzi

8. Mlinzi wa mlango huitwaje?

  1. Boharia
  2. Baharia
  3. Bawaba
  4. Banati
  5. Bawabu

9. Neno lipi tofauti na mengine katika maneno yafuatayo?

  1. Maji
  2. Maziwa
  3. Soda
  4. Juisi
  5. Samli

10. Nywele zinazoota kuanzia kwenye maskio mpaka kwenye mashavu huitwa?

  1. Mvi
  2. Sharafa
  3. Ndevu
  4. Sharubu
  5. Kope

11. Sehemu ngo’mbe huogeshwa hili kuwaepusha na magonjwa hutwa?

  1. Mto
  2. Ziwa
  3. Bwawa
  4. Josho
  5. Joshi

12. Joshua yupo jikoni anapaa samaki. Neno anapaa kama lilivyo tumika katika sentensi lina maana gani?

  1. Kuwapaka samaki chumvi
  2. Kuondoa magamba ya samaki
  3. Kuondoa mifupa katika samaki
  4. Kukausha samaki kwa moto
  5. Kuwakata samaki vipande vipande.

13. Siku ya nne baada ya leo huitwa?

  1. Mtondo
  2. Mtondo kutwa
  3. Mtondogoo
  4. Kesho kutwa
  5. Mtondogoo kutwa

14. Msemo usemao “kushikwa sikio” una maana ipi?

  1. Kusemwa
  2. Kunong’onezwa
  3. Kuelezwa
  4. Kusengenywa
  5. Kuonywa

15. “Bwana mkubwa amelala ndani lakini ndevu zipo nje zapepea” Jibu sahii la kitendawili hiki ni

  1. Ulezi
  2. Mpunga
  3. Ngano
  4. Mahindi
  5. Mtama

16. Kisawe cha eupe ni kipi?

  1. Chokaa
  2. Angavu
  3. Theluji
  4. Ukunga
  5. Angaza

17. Kimatu ni motto wa nani?

  1. Nzige
  2. Nyuki
  3. Inzi
  4. Kipepeo
  5. Buibui

18. Kitenzi “piga” kikiwa katika hali ya kutendeka kitakua neon lipi?

  1. Pigia
  2. Pigwa
  3. Pigika
  4. Pigiwa
  5. Pigana

19. “Sote tunafanya mtihani darasani” Neno darasani limetumika kama aina gani ya neon?

  1. Kielezi
  2. Kivumishi
  3. Kitenzi
  4. Kiwakilishi
  5. Nomino

20. Ni sentensi ipo sahii kimuundo katika zifuatazo?

  1. Amenunua gari mashaka
  2. Mashaka gari amenunua
  3. Amenunua mashaka gari
  4. Mashaka amenunua gari
  5. Gari amenunua mashaka.

SEHEMU B. LUGHA YA KIFASIHI.

Katika swali la 21-30, andika jibu sahili la kila swali.

21. Watoto wa mfalme ni rahisi kujificha” Jibu la kitendawili hiki ni………..

  1. Macho
  2. Vifaranga
  3. Siafu
  4. Mvi
  5. Sungura

22. Kamili methali. “Heri kufa macho kuliko…………

  1. Kujikwaa ulimi
  2. Kuumia moyo
  3. Kuzama majini
  4. Kufa moyo
  5. Kufa jicho moja

23. Anatengeneza mchuzi mtamu sana lakini hapiki jikoni. Lipi jibu la kitendawili hiki?

  1. Ng’ombe
  2. Nyuki
  3. Mbuzi
  4. Muwa
  5. Kuku

24. Nimeugua kwa muda mrefu sana, lakini sasa ni…………wa afya. Neno lipi linakamilisha sentensi hii?

  1. Hoi
  2. Buheri
  3. Buheli
  4. Mzuri
  5. Mwingi

25. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

  1. Mbalika
  2. Nzi
  3. Mhindi
  4. Embe
  5. Mtama

26. Kamilisha methali hii.Mwamba ng’oma……………

  1. Hualika watu wengi
  2. Hufanya maandalizi mengi
  3. Huimba nyimbo nyingi
  4. Ngozi huvutia kwake
  5. Hucheza na jamaa zake

27. Tegua kitendawili kifuatacho. “Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji”

  1. Kikombe
  2. Kata
  3. Kinywa
  4. Kibatari
  5. Mtungi

28. Ni methali ipi kati ya hizi inafanana na isemayo, mwenda pole hajikwai?

  1. Haba na haba hujaza kibaba
  2. Fuata nyuki ule asali
  3. Awali ni awali hakuna awali mbovu
  4. Mchumia juani hulia kivulini
  5. Baada ya dhiki faraja

29. Methali isemayo, “mgaagaa na upwa hali wali mkavu inatoa funzo gani?

  1. Bidii huleta maafanikio
  2. Mafanikio ni matokeo ya kazi
  3. Bidii huleta faraja
  4. Bidii ni kazi ya kuhangaika
  5. Mafanikio ni ya lazima.

30. Methali ipi kati ya hizi  haitoi onyo kuhusu tabia ya mtu?

  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
  2. Kiburi si maungwana
  3. Motto mkaidi mngoje siku ya ngoma
  4. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi
  5. Mt0to mwerevu hafunzi adabu

SEHEMU C. UFAHAMU.

Soma kifungu kifuatacho kwa makini kasha jibu maswali 31-40.

Jua lilikuwa linaunguza mithili ya moto. Hapakuwa na nyasi wala miti iliyokuwa na majani ya rangi ya kijani.Kila uoto ulikuwa wa rangi ya kahawia kavu! Aidha kupata tone la maji ya kunywa ilikuwa ndoto kwani mito na visima vyote vilikauka kau.Baada https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image073.jpgkuhangaika kwa njaa na kiu, ndipo wanyama waliamua waitishe mkutano ili wajadili hatua ya kuchukua. Makundi • ya wanyama wa aina mbalimbali walikutana chini ya mbuyu. Swala, nyani, mbawa na tembo wote walikuwepo.

"Kama mjuavyo mimi ndimi mfalme wa wanyama wote.Niungurumapo hapana achezae kwa hiyo bila shaka mtakubali kuwa mimi ndiye mwenyekiti wa mkutano huu."alitangaza simba.Wanyama wote walitazamana na kutikisa vichwa kwa ishara ya kuafiki. Kisha alisimama na kusema "Mheshimiwa mwenyekiú, jana nilisikia mlindimo toka upande wa magharibi. Hivyo ninashauri sote tuhame na kuelekea upande huo ili tuokoe maisha yetu kwani huko kuna dalili ya mvua."Wanyama wote waliunga mkono hoja hiyo,isipokuwa kobe ambaye alisema, "mheshimiwa mwenyekiti, endapo kweli tumeazimia kuhama, sisi akina kobe tunaomba mtubebe kwani kasi yetu ya kutembea ni ndogo mno."

Baada ya kila mnyama kutoa rai yake ,Mwenyekiti alisimama na kusema, "Nimesikia yote mliyosema, kabla ya kuanza kuhama nakutuma wewe ngombe upeleke ujumbe wetu kwa binadamu ili waache kuharibu mazingira, kwani hicho ndicho kiini cha matatizo yanayotusibu.Wewe ni kiungo baina yetu na binadamu." ngombe alikubali.

Baada ya kufika ujumbe ule, binadamu alijibu kuwa alikwishaelewa tatizo Ia mazingira na tayari alikuwa na mpango kabambe wa kuchinja mifugo yote ili kutekeleza ushauri wa wataalamu wa mazingira wa kuiokoa dunia na janga Ia jangwa. Kusikia hivyo ngombe alichanja mbuga kuelekea kwa wanyama wengine.

31.  Kwa mujibu wa habari uliyo soma, mkutano wa wanyama ulifanyika wapi?

  1. Kwa mfalme
  2.  Kisimani
  3. Chini ya mbuyu D. 
  4. Kwenye majani
  5. Jangwani.

32.  Mwenyekiti wa mkutano wa wanyama alikuwa nani?

  1. Ng ombe
  2.  Kobe
  3. Nyati
  4. Simba
  5. Nyani

33. Hali ya kukauka kwa mito,visima nyasi na miti kunakutokana na ukosefu wa mvua inaitwaje?

  1. Ukame
  2. Uoto https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image049.jpg
  3.  Kahawia https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image011.jpg
  4.  loto
  5. Janga.

34. Jina lingine Ia mnyama aliye washauri wanyama wote kuhamia upande ambako kulikuwa na dalili ya mvua ni lipi kati ya https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image042.jpgyafuatayo.

  1.  Ndovu B.
  2.  Ngwena
  3. Mbega 
  4.  Kima
  5. Mbogo.

35.Katika habari uliyo soma sababu iliyomfanya kobe kutoafiki moja kwa moja hoja ya kuhama ni ipi?

  1. alikuwa mpinzani wa mwenyekiti ,
  2. aliogopa kuachwa nyuma, https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image022.jpg
  3. kulikuwa na jua kali
  4. wanyama wengine wangeweza kumla,
  5. kobe ni mvivu kutembea.

36. kwa mujibu wa habari hii ,uharibifu mkubwa wa mazingira hufanywa na nani?

  1. tembo
  2.  mbawala
  3.  swala https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image083.jpg
  4. binadamu
  5.  nyani.

37. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno janga?

  1. Maafa 
  2.  Kiu https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image062.jpg
  3. Ukame 
  4. angwa 
  5. Joto.

38.  Kifungu cha maneno "alichanjambuga"kinamaana gani?

  1. Alijirudi
  2. Alitembea
  3. Alikimbia
  4. Alirudi https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image056.jpg
  5. Aliruka

39.  Binadamu alikusudia kuchinja wanyama wa aina gani

  1. Wanyama pori wote
  2. Ngombe na simba  https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image056.jpg
  3. Wanyama wadogo wote
  4. Wanyama wakubwa wote
  5. Wanyama wote wanaofugwa

40.  Kichwa cha somo uliyosoma kingefaa kiwe kipi?

  1. Kiangazi na jangwa
  2. Matatizo ya binadamu
  3. Jua kali
  4.  Uhamisho wa wanyama
  5. Uharibifu wa mazingira 

SEHEMU D. USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuweka kivuli katika herufiya jibu.

Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali,

Mule wanamotangaza, matangazo lugha mbili, Juu kuwa Kingereza, Chini kuwa Kiswahili, Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Kitangazwe Kingereza, baada ya Kiswahili

Hivi tutapotimiza, lugha itakuwa ghali,

Hivi mnavyofanyiza, sana mnaidhalili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Serikali bembeleza, tafakari tafadhali,

Jambo hili kueleza, kwa zingine serikali Kiswahili kutangaza, kuwa Chini twakidhili Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Tuache kukipumbaza, kwa andiko au kauli, Kwa nyuma kukisogeza, kukipa kisulisuli,

Lazima kuyafukuza, yawezayo kikatili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Na wenyewe kujikaza, kwa bidii za kimwili kiswahili kutukuza, tukivalie bangili,

Ngomani kutumbuiza, waume na wanawali Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

41. Katika shairi hilo mstari wa pili katika ubeti wa pili una mizani mingapi?

  1. Tano
  2. mbili
  3. kumi na sita
  4. nane
  5. thelathini na tatu

42. Katika ubeti wa nne, vina ni vipi?

  1. Za na li 
  2. La na li
  3. La na ya
  4. Ju na za
  5. Tu na li

43.      Kituo ni kipi katika shairi hili?

  1. Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali
  2.  Kitangazwe Kingereza, badala ya Kiswahili 
  3. Serikali bembeleza, tafakari tafadhali
  4. Tuache kukipumbaza, kwa andiko na kauli
  5. Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

44.      Shairi hili linahimiza kuhusu nini?

  1. Kudumisha na kuendeleza mila
  2. Kudumisha na kuendeleza jadi zetu
  3. Kudumisha lugha ya Kingereza
  4.  Kudumisha na kuendeleza Kiswahili 
  5.  Kudumisha na kuendeleza lugha

45.      Ujumbe unaopatokana katika shairi hili unafanana na methali ipi?

  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
  2.  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  3. Mkono usioweza kuukata ubusu. 
  4.  Ukitaka cha uvunguni sharti uiname.
  5. Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.

46.      Kutokana na shairi ulilosoma neno "kutukuza” lina maana ipi?

  1. Shutumu 
  2.  Laumu
  3. Heshimu 
  4. Fadhaisha
  5. Kasirisha

 SEHEMU D. UTUNGAJI

Panga sentensi nne (4) zifuatazo hili ziwe kwa mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B,C na D.

47. Zizi hilo limegawanywa katika sehemu mbili

48. Baba yangu anafuga mbuzi Ng’ombe na kondoo

49. Nje ya nyumba yetu kuna zizi kubwa

50. Sehemu moja ni ya ngo’ombe na nyingine ni ya mbuzi na kondoo.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 8

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI YA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA SABA

MUDA: 2:30 

KISWAHILI

MAELEZO KWA MTAHINIWA

  1. Mtihani huu unamaswali 50
  2. Jibu Maswali Yote
  3. ANDIKA Majibu yako kwa Herufi kubwa
  4. Hakikisha kazi yako inasomeka vyema

SEHEMU A: SARUFI

 Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufl ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia 

1.Neno lipi kati ya haya lina maaana sawa na shari?

  1.  Ubunifu
  2. Umaarufu
  3. Uzembe
  4. Ugomvi
  5. Uzushi

2.      Shida alivaa nguo za kijeshi wakati wa mkutano.Neno "za kijeshi" ni aina gani ya neno?

  1. Kivumishi
  2. Kielezi
  3. Kitenzi
  4. Kiwakilishi 
  5.  Nomino

3.      Hicho ulichopata sikupata lakini nimepata hiki" katika sentensi hii, maneno "hicho na hiki"ni aina gani ya maneno?

  1. Vivumishi 
  2. Viwakilishi
  3. Vielezi    
  4. Vitenzi
  5. Nomino

 4.      Ni sentensi ipi iliyo sahihi kimuundo  kati ya zifuatazo?

  1. Amenunua gari mashaka
  2. Mashaka gari amenunua 
  3. Amenunua mashaka gari 
  4. Mashaka amenunua gari
  5. Gari amenunua mashaka.

5.      Maana ya neno "faraghani" ni ipi kati ya hizi?

  1. Wazi wazi
  2. Kivulini
  3. Pembejeo
  4. Mafichoni
  5. Hadharani

6.      Wingi wa sentensi "Mbuzi wamepotea" ni upi?

  1. Mbuzi zetu zimepotea
  2. Mbuzi yetu zimepotea
  3. Mbuzi wetu wamepotea 
  4.  Mbuzi zetu wamepotea
  5. Mbuzi yetu wamepotea.

7.   Kinyume cha neno "duwaa" ni kipi?

  1. Shangaa
  2. Staajabu
  3.  Bashasha
  4. Pumbaa
  5.  Butwaa

8.  "Uvumilivu ulimfanya Pendo apate zawadi. "Uvumilivu ni aina gani ya neno?

  1. Nomino
  2.  Kitenzi
  3. Kivumishi
  4. Kihisishi
  5. Kiwakilishi

9.       Yupi kati ya wafuatao ni lazima awe mwanaume?

  1. Mjomba 
  2. Binamu
  3. Mjukuu
  4.  Ndugu 
  5. Mzee

10. "Walimu watafundisha masomo yao vizuri". Sentensi hii ipo katika wakati gani?

  1. Uliopita 
  2.  Ujao
  3. Uliopo
  4. Mazoea
  5. Timilifu

11.     "Wanafunzi hodari watapewa zawadi". Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?

  1. Ujao 
  2.  Timilifu 
  3. Uliopita   
  4.  Mazoea 
  5. Uliopo

12.     Maji yamejaa "pomoni" Neno "pomoni" ni aina ipi ya neno?

  1. Nomino  
  2.  Kiwakilishi   
  3. Kielezi
  4. Kihisishi  
  5. Kivumishi

13.     Kati ya maneno "Sherehi, Sherehe, Shamrashamra, Hafla, Tafrija" neno lipi halihusiani na mengine?

  1. Sherehi  
  2. Sherehe 
  3.  Shamrashamra 
  4. Hafia 
  5. Tafrija

14.     Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na "thubutu"?

  1. Ufidhuli  
  2. Ujasiri 
  3. Umahiri 
  4. Ukakamavu 
  5. Utashi

15."Kuzua kizaazaa" ni msemo wenye maana gani?

  1. Ushabiki   
  2. Upendeleo
  3. Malumbano
  4. Masikitiko  
  5. Majungu 

16, "Mlima meru unafuka moshi" Ukanusha wa sentensi hii ni upi?

  1. Mlima meru unawaka moshi
  2. Mlima meru unatoa moshi.
  3. Mlima meru unafukiza moshi D. 
  4. Mlima meru haufuki moshi 
  5. Mlima meru hauwaki moshi.

17.       Panga maneno yafuatayo kwa kuanzia na neno ambalo katika familia hiyo linaonesha aliyetangulia kuzaliwa hadi wa mwisho kuzaliwa: Baba, kitukuu, babu, kilembwe, mjukuu, kilembwekeza.

  1. Babu, Baba, Mjukuu, Kitukuu,Kilembwe, Kilembwekeza
  2.  Baba, mjukuu, kitukuu, kilembwe,  kilembwekeza, babu
  3. Kilembwekeza, kitukuu, mjukuu, bab babu, kilembwe
  4. Babu, mjukuu, kitukuu, kilembwe, kilembwekeza, baba
  5. Mjukuu, kitukuu, baba, babu, kilembwe, kilembwekeza

18. Katika vitenzi "sitafyeka" na "hupendi" ni silabi zipi zinazoonesha ukanushi?

  1. ta na hu
  2. ta na pe
  3. ka na ndi 
  4.  si na hu
  5. fye na pe.

19. Neno lipi kati ya haya halilandani na mengine?

  1. Cheka
  2. Tabasamu
  3. Furaha 
  4.  Sherehe 
  5.  Shere.

20.   Ni methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza ushirikiano katika jamii?

  1. Chanda chema huvikwa pete
  2. Mchumajanga hula na wa kwao
  3. Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu
  4. Mwenda pole hajikwai
  5.  Wapishi wengi huharibu mchuzi

20.   Ni methali ipi kati ya zifuatazo inahimiza ushirikiano katika jamii?

  1. Chanda chema huvikwa pete
  2. Mchumajanga hula na wa kwao
  3. Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu
  4. Mwenda pole hajikwai
  5. Wapishi wengi huharibu mchuzi

21.      Methali isemayo, "Katika msafara wa mamba na kenge wamo" iko sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?

  1. Akutukanaye hakuchagulii tusi. 
  2.  Kila kiboko na kivuko chake.
  3. Amulikaye nyoka huanzia miguuni mwake. 
  4. Tajiri na mali yake maskini na mwanawe. 
  5.  Hakuna masiki yasiyo na mbu.

22.      Diengi anapenda kuwarairai watu. "l<urairai watu" ni msemo wenye maana ipi?

  1. Kuwasihi watu ili apate cheo anachokipenda
  2. Kusema na watu kwa maneno mazuri
  3. Kusema na watu ili uwape chochote
  4.  Kusema kwa watu kwajili ya kuwatapeli
  5. Kuwabembeleza watu ili wasimpangie kazi

23.      Msemo "kubarizi" maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya .

  1. Sherehe 
  2.  mkutano 
  3.  mazungumzo ya kawaida 
  4. burudani 
  5.  chakula cha pamoja

24.      Methali isemayo "Kila mtoto na koja lake" ina maana gani? 

  1. Kila binadamu ana mapungufu yake.
  2.  Kila mtoto ana matatizo yake.  
  3. Kila mtoto ana mapungufu yake. 
  4.  Kila mtoto ana wazazi wake.  
  5. Kila binadamu ana tabia yake.

Nahau isemayo "kuvishwa kilemba cha ukoka" ina maana gani?

  1. Kupewa sifa unazostahili 
  2.  Kupewa sifa mbaya 
  3.  Kupewa sifa nyingi 
  4.  Kupewa sifa chache
  5. Kupewa sifa usizostahili

26.   "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa ulimwengu." Ni methali ipi inafanana na methali hii?

  1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
  2. Asiye na mwana aelekee jiwe 
  3. Asiye na bahati habahatishi
  4. Asiyejua kufa atazame kaburi
  5. Asiyekubali kushindwa si mshindani.

27.   "Haba na haba hujaza kibaba" Methali hii inatoa funzo gani?

  1. Umuhimu wa kupima vitu
  2. Tunajiwekea akiba
  3. Vitu hupimwa na kibaba tu 
  4. Tunapawa kupima vibaba 
  5.  Kibaba hujaza vitu.

28.   "Heri kufa macho kuliko ……………."Methali hii UKAMILISHWA na kifungu kipi cha maneno?

  1. kujikwaa ulimi
  2. kuumia moyo
  3. kuzama majini
  4. kufa moyo
  5. kufa jicho moja

29.   "Maji yakimwagika hayazoolekl hii ina maana gani kati ya zifuatayo?

  1. Ukitaka usizoe maji,usimwage
  2. Tuwe waangalifu katika kutenda jambo
  3. Tuwe waangalifu tunapobeba maji
  4. Maji yakimwagika hugeuka matope
  5. Jambo lililoharibika halitengenezeki

30.   "Amani haiji kifungu hiki cha maneno kinakamilisha methali usahihi?

  1. ila kwa mzozo mkubwa
  2. ila kwa malumbano makali
  3.  bila kuwa na imani 
  4. ila kwa ncha ya upanga 
  5. bila makubaliano.

30.   "Amani haiji kifungu hiki cha maneno kinakamilisha methali usahihi?

  1. ila kwa mzozo mkubwa
  2. ila kwa malumbano makali
  3.  bila kuwa na imani 
  4. ila kwa ncha ya upanga 
  5. bila makubaliano.

SEHEMU C. UFAHAMU.

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31-40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

Jua lilikuwa linaunguza mithili ya moto. Hapakuwa na nyasi wala miti iliyokuwa na majani ya rangi ya kijani.Kila uoto ulikuwa wa rangi ya kahawia kavu! Aidha kupata tone la maji ya kunywa ilikuwa ndoto kwani mito na visima vyote vilikauka kau.Baada ya kuhangaika kwa njaa na kiu, ndipo wanyama waliamua waitishe mkutano ili wajadili hatua ya kuchukua. Makundi  ya wanyama wa aina mbalimbali walikutana chini ya mbuyu. Swala, nyani, mbawa na tembo wote walikuwepo. 

"Kama mjuavyo mimi ndimi mfalme wa wanyama wote.Niungurumapo hapana achezae kwa hiyo bila shaka mtakubali kuwa mimi ndiye mwenyekiti wa mkutano huu."alitangaza simba.Wanyama wote walitazamana na kutikisa vichwa kwa ishara ya kuafiki. Kisha alisimama na kusema "Mheshimiwa mwenyekiú, jana nilisikia mlindimo toka upande wa magharibi. Hivyo ninashauri sote tuhame na kuelekea upande huo ili tuokoe maisha yetu kwani huko kuna dalili ya mvua."Wanyama wote waliunga mkono hoja hiyo,isipokuwa kobe ambaye alisema, "mheshimiwa mwenyekiti, endapo kweli tumeazimia kuhama, sisi akina kobe tunaomba mtubebe kwani kasi yetu ya kutembea ni ndogo mno."

Baada ya kila mnyama kutoa rai yake ,Mwenyekiti alisimama na kusema, "Nimesikia yote mliyosema, kabla ya kuanza kuhama nakutuma wewe ngombe upeleke ujumbe wetu kwa binadamu ili waache kuharibu mazingira, kwani hicho ndicho kiini cha matatizo yanayotusibu.Wewe ni kiungo baina yetu na binadamu." ngombe alikubali.

Baada ya kufika ujumbe ule, binadamu alijibu kuwa alikwishaelewa tatizo Ia mazingira na tayari alikuwa na mpango kabambe wa kuchinja mifugo yote ili kutekeleza ushauri wa wataalamu wa mazingira wa kuiokoa dunia na janga Ia jangwa. Kusikia hivyo ngombe alichanja mbuga kuelekea kwa wanyama wengine.

31.  Kwa mujibu wa habari uliyo soma, mkutano wa wanyama ulifanyika wapi?

  1. Kwa mfalme
  2.  Kisimani
  3. Chini ya mbuyu D. 
  4. Kwenye majani
  5. Jangwani.

32.  Mwenyekiti wa mkutano wa wanyama alikuwa nani?

  1. Ng ombe
  2.  Kobe
  3. Nyati
  4. Simba
  5. Nyani

33. Hali ya kukauka kwa mito,visima nyasi na miti kunakutokana na ukosefu wa mvua inaitwaje?

  1. Ukame
  2. Uoto
  3.  Kahawia
  4.  Loto
  5. Janga.

34. Jina lingine Ia mnyama aliye washauri wanyama wote kuhamia upande ambako kulikuwa na dalili ya mvua ni lipi kati ya yafuatayo.

  1.  Ndovu B.
  2.  Ngwena
  3. Mbega 
  4.  Kima
  5. Mbogo.

35.Katika habari uliyo soma sababu iliyomfanya kobe kutoafiki moja kwa moja hoja ya kuhama ni ipi?

  1. alikuwa mpinzani wa mwenyekiti ,
  2. aliogopa kuachwa nyuma,
  3. kulikuwa na jua kali
  4. wanyama wengine wangeweza kumla,
  5.  kobe ni mvivu kutembea.

36. kwa mujibu wa habari hii ,uharibifu mkubwa wa mazingira hufanywa na nani?

  1. tembo
  2.   mbawala
  3.   swala
  4. binadamu
  5.   nyani.

37. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno janga?

  1. Maafa 
  2.   Kiu
  3.  Ukame
  4. Jangwa 
  5.  Joto.

38.  Kifungu cha maneno "alichanjambuga"kinamaana gani?

  1. Alijirudi
  2. Alitembea
  3. Alikimbia
  4. Alirudi
  5. Aliruka

39.  Binadamu alikusudia kuchinja wanyama wa aina gani

  1. Wanyama pori wote
  2. Ngombe na simba  
  3. Wanyama wadogo wote
  4. Wanyama wakubwa wote
  5. Wanyama wote wanaofugwa

40.  Kichwa cha somo uliyosoma kingefaa kiwe kipi?

  1. Kiangazi na jangwa
  2. Matatizo ya binadamu
  3. Jua kali
  4.  Uhamisho wa wanyama
  5. Uharibifu wa mazingira

SEHEMU D. USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa Kuweka kivuli katika herufi ya jibu.

Mtu kujitegemea, huwajambo Ia lazima,

Usipende subiria, kusaidiwa daima,

Huwezi kuendelea, ndugu usipojituma,

Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema, Fedheha kuombaomba, takuwa mtu wa nyuma, Hutakuja kujigamba, ukikudharau umma. Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Kazi mtu usidhani, sharti niya kusoma,

Ya kuleta ofisini, na kuhesabu ndarama,

Waweza kwenda shambani, ushikejembe kulima, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima,

Pengine uitwe mwizi, umezoea dhuluma, Wajapo wapelelezi, ndiwe watakuandama, Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

41.      Katika shairi ulilosoma neno "ndarama" lina maana ipi? 

  1. Mali
  2. Pesa
  3.  Gharama
  4. Amana
  5. Thamani

42.      Kisawe cha neno "taadhima" ni kipi? 

  1. Heshima
  2. Taashira
  3. Dhamiri
  4. Dhima
  5. Dhamana

43.      Ujumbe unaopatikana katika shairi hili unaweza kuwasilishwa kwa methali ipi kati ya zifutazo? ........

  1. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi 
  2. Mchagua jembe si mkulima
  3. Mkulima hasahau jembe kiserema 
  4.  Mkulima halaumu jembe lake
  5. Kilimia kikizama kwa jua huibuka

44.      Katika shairi ulilosoma kituo bahari ni kipi? 

  1. Mtu kujitegemea, huwa jambo la lazima. 
  2.  Kama Mungu kakuumba, mzima huna kilema.
  3. Utaambiwa doezi, mtu uso taadhima.
  4. Waweza kwenda shambani, ushike jembe kulima 
  5.  Kamwe hupati heshima, usipojitegemea.

45.      Katika shairi ulilosoma nusu mstari una mizani ngapi? 

  1. Nane
  2. Mbili
  3. Tatu
  4.  Nne
  5. Kumi na tano

46.      Neno "fedheha" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

  1.  Maudhui
  2. Lawama
  3. Adibu
  4.  Adhibu 
  5.  Aibu

SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katikaswali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo iii ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A,B,C na D. Andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.

47.Kwa njia hii, vizazi vilivyofuata viliweza kujua uvumbuzi uliofanywa kabla yao.

48. Jambo muhimu lililofanywa na mababu zetu ni kuhifadhi kumbukumbu za uvumbuzi waokwa kuchora kila kifaa walichovumbua.

49. Kwa kutumia vizazi vilivyotangulia nasi pia tunaweza kuvumbua vitu vipya ambavyovitaweza kutuletea maendeleo zaidi.

50. Hivyo maisha ya binadamu yakaendelea kuwa bora na yenye manufaa kila siku.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZKISWAHILI STANDARD SEVEN EXAM SERIES 4

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256